Kwa kuhudhuria kiongozi wa kisheria: Atabatu Abbasiyya tukufu yahitimisha mashindano ya Qur’an tukufu ya kwanza kitaifa…

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’an tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya uislamu na ubinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imekamilisha mashindano ya kwanza ya Qur’an tukufu baada ya kumaliza hatua ya utangulizi iliyo husisha wasichana 200 walio hifadhi Qur’an kutoka katika mikoa mbalimbali ya Iraq, na kuchaguliwa wasichana 52 walio shindanishwa siku mbili katika ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya kwa ajili ya kuwapata washindi, pia shindano hilo ni sehemu ya kukamilisha mfululizo wa mashindano yaliyo simamiwa na Maahadi katika mkoa wa Najafu na matawi yake yaliyopo katika mikoa mingine, yanayo lenga kueneza utamaduni wa Qur’an na kukomaza uhusiano wa kiroho pamoja na kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu katika maisha ya kila siku pia ni sehemu ya kushajihisha usomaji wa Qur’an.

Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu, Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi katika ujumbe wake aliotoa, ameshajihisha kuendeleza harakati hizi na kuhakikisha mashindano ya Qur’an hayahusishi wanaume peke yao, bali yahusishe pia wanawake na washajihishwe kuihifadhi pamoja na kuisoma kwa mazingatio jambo litakalo saidia kua na kizazi kinacho fuata utamaduni wa Qur’an chenye tabia nzuri na chenye kujitambua”.

Mashindano haya yaliyo dumu siku mbili, yalihusisha walio hifadhi juzuu tatu za mwanzo, kisha wa juzuu tano, kisha wa juzuu kumi na walio hifadhi juzuu ishirini.

Siku ya pili, walimalizia mashindano na kufanya hafla ya kufunga mashindano ambayo ilienda sambamba na kutoa zawadi kwa washindi wa kwanza katika kila kikundi, pamoja na kugawa zawadi kwa jopo la majaji na msomaji wa kike wa Maahadi ya Qur’an tukufu (Hauraa Aamir) kwa kushika nafasi ya kwanza katika mashindano matatu ya Qur’an ya kitaifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: