Wahandisi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wakamilisha ujenzi wa madarasa mawili katika chuo kikuu cha Basra…

Maoni katika picha
Wahandisi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu wamekamilisha mradi wa ujenzi wa madarasa mawili katika chuo kikuu cha Basra –kitivo cha malezi ya elimu ya kibinadamu- kitengo cha maarifa ya Qur’an, kazi ilianza mara moja baada ya makubaliano yaliyo fanyika na uongozi mkuu wa Ataba tukufu, kufuatia maombi yaliyo letwa na chuo hicho kwa kitengo cha usimamizi wa kihandisi.

Yamejengwa madarasa mawili yenye ukubwa wa mt(16x6), na urefu wa kwenda juu wa mt (3,5), na paa ya pili ya (PVC) iliyo tengenezwa na Kashi, ukuta wote umefunikwa kwa (PVC) sm (60x60) na wameweka milango, madirisha na umeme, pamoja na kusakafia njia za nje pamoja na maeneo yanayo zunguka madarasa hayo, wamejenga kwa kufuata maelekezo waliyo kubaliana na wanufaika wa mradi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: