Chini ya kauli mbiu isemayo (Kwa utukufu wa damu za mashahidi wetu tumepata ushindi), Chuo kikuu cha Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya mahafali ya kusherehekea ushindi wa Iraq ulio fanikishwa na wanajeshi wa serikali pamoja na wapiganaji wa Hashdi Sha’abi kwa kukomboa ardhi yote iliyo kua imetekwa na magaidi wa Daesh, mahafali hiyo imefanywa katika uwanja wa chuo, imekua na mahudhurio makubwa ya wakufunzi na viongozi wa idara pamoja na wawakilishi wa vitengo mbalimbali na kundi kubwa la wanafunzi.
Baada ya kusomwa Qur’an tukufu na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, na kuimbwa wimbo wa taifa, mkuu wa chuo kikuu cha Ameed Dokta Jaasim Marzuki aliwasilisha ujumbe wake, alianza kwa kumpongeza Marjaa dini mkuu na watu wa Iraq kutokana na ushindi huu, akasema kua: “Hakika leo chuo chetu kinasherehekea ushindi mkubwa uliopatikana kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na kujitolea muhanga kwa wanajeshi wetu watukufu na Hashdi Sha’abi, hakika walijitolea kila kitu kwa ajili ya kulinda ardhi yao na maeneo matakatifu”.
Akaongeza kusema kua: “Hakika chuo kikuu cha Ameed kutoa zawadi kwa watoto wa mashahidi ni sehemu ndogo sana ya wajibu wetu tunao paswa kumfanyia mtu aliye jitolea kila alicho nacho kwa ajili ya kukomboa ardhi ya Iraq kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh”.
Mahafali ilihusisha vitu vingi, ikiwa ni pamoja na kulaani msimamo wa Marekani wa kuitambua Qudsi kama mji mkuu wa Israeel, na ziliimbwa kaswida mbalimbali zilizo husu uzalendo na kuipenda nchi na kupongeza ujasiri wa wapiganaji watukufu, hali kadhalika wanafunzi walifanya igizo kuhusu umoja wa taifa, na namna umoja huo ulivyo kua nyenzo muhimu ya kuzishinda njama za magaidi.
Na mwisho kabisa wakapewa zawadi watoto wa mashahidi walio sababisha kupatikana kwa ushindi huu mtukufu.