Waziri wa mambo ya ndani wa Iraq Ustadh Qassim A’araji ametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu, baada ya kamaliza kufanya ziara na kuomba dua alikutana na kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na wakaongelea mambo mbalimbali yakiwemo kuhusu ushindi wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi kwa kukomboa ardhi yote ya Iraq kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh, ushindi uliopatikana kutokana na baraka za fatwa tukufu iliyo tolewa na Marjaa dini mkuu katika mji mtukufu wa Najafu, (fatwa ya jihadi ya kujilinda) na namna wananchi walivyo iitikia, wakakubaliana kuenzi ushindi huu kwa kupambana na fikra za ubaguzi na misimamo mikali, pamoja na kuwajali majeruhi na familia za mashahidi.
Pia waziri wa mambo ya ndani alipata fursa ya kutembelea mitambo ya kamera za ulinzi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na akapewa maelezo kwa ufupi na kiongozi wa idara ya mawasiliano ya Atabatu Abbasiyya Muhandisi Farasi Abbasi Hamza kuhusu utendaji wa mitambo hiyo, na mafanikio yaliyo patikana kutokana na utendaji wa mitambo hiyo katika kudhibiti usalama na kuhesabu mazuwaru (watu wanaokuja kufanya ziara).
Waziri wa mambo ya ndani alisifu utendaji wa mitambo hiyo ya kisasa pamoja na wasimamizi wa mitambo, akasisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano baina ya jeshi la serikali na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kulinda amani katika mkoa mtukufu wa Karbala.