Mwezi kumi Rabiu-Thani ni siku aliyo fariki bibi Fatuma Maasuma bint wa Imamu Mussa Kaadhim (a.s)…

Maoni katika picha
Mwezi kumi Rabiu-Thani inasadifu siku aliyo fariki bibi Fatuma Maasuma bint wa Imamu Mussa Kaadhim na dada wa Imamu Ridha (a.s), alifariki mwaka wa 201h, katika mji wa Qum, akiwa na umri usiozidi miaka ishirini na nane kama ilivyo kuja katika riwaya, katika muda mfupi huo wa uhai wake alipatwa na mitihani na misukosuko mingi kama ile aliyo pata shangazi yake Aqila Bani Hashim Zainabu Kubra (a.s), hakika alifungua macho yake hapa duniani baba yake akiwa jela, zilikua zama zilizojaa mateso na ukatili kutoka kwa utawala wa bani Abbasi na alivuminia dhulma nyingi.

Kukua kwake (a.s).

Haruna Rashidi alijalia kukua kwake kuwe chini ya usimamizi wa kaka yake Imamu Ridha (a.s), kwa sababu mwaka wa kuzaliwa kwake baba yake alitiwa jela, kisha akapewa sumu na akafariki mwaka wa 183h, hivyo aliishi pamoja na ndugu zake chini ya usimamizi wa kaka yake Imamu Ridha (a.s).

Safari yake (a.s) ya kwenda Khurasani.

Yeye pamoja wa familia nzima ya Abu Twalib (a.s) walipata wasiwasi kubwa kuhusu usalama wa Imamu Ridha (a.s) alipo itwa na Ma-amun huko Khurasani, baada ya kuambiwa na kaka yake Imamu Ridha (a.s) kua atauawa katika safari hiyo huko Tusi, akaamua kufunga safari na kumfuata.

Safari yake (a.s) ya kwenda Qum.

Aliondoka (a.s) akimfuata kaka yake Imamu Ridha (a.s), akiwa na matumaini ya kukutana naye akiwa hai, hakika safari ilikua ndefu, akaugua na akashindwa kuendelea na safari, akauliza umbali uliobaki kufika katika mji wa Qum –kipindi hicho alikua amefika katika mji wa Saawah- akaambiwa kuna umbali wa Farsakh kumi, sawa na kilometa 70, akaamrisha apelekwe katika mji wa Qum.

Kuwasili kwake (a.s) katika mji wa Qum.

Alibebwa (a.s) na kupelekwa katika mji wa Qum akiwa mgonjwa, alipo wasili, alipokelewa na viongozi wa mji huo, wakiongozwa na Mussa bun Khazraj bun Sa’adi Ash’ariy, akashika kamba ya ngamia wake na akamuongoza hadi nyumbani kwake, aliishi katika nyumba hiyo hadi alipo fikwa na umauti baada ya siku 17, akaoshwa na kuvishwa sanda kisha akaswaliwa na kuzikwa sehemu ambapo kaburi lake lipo hadi sasa, baada ya kuzikwa kaburi lake likajengewa banda, hadi alipo kuja bibi Zainabu mtoto wa Imamu Muhammad Jawaad (a.s) na kumjendea Kubba.

Tarehe ya kufariki kwake (a.s).

Bibi Fatuma aliishi siku 17 katika mji wa Qum, alizitumia kwa kufanya ibada na kusoma dua, katika mahala palipo julikana kwa jina la (Baitu Nuur) sasa hivi nyumba hiyo ipo katika eneo linalo itwa mji wa Satiih, alifariki mwezi kumi Rabiu-Thani, (Au mwezi kumi na mbili kwa mujibu wa baadhi za riwaya), alifariki kabla hajakutana na kaka yake, jeneza lake lilishindikizwa na watu wengi sana, mji mzima ulizizima kutokana na huzuni ya kifo chake, wakaenda kumzika katika makaburi ya Babalan sehemu ambapo kaburi lake lipo hadi sasa.

Fadhila za kumzuru (a.s).

Kuna riwaya nyingi zinazo elezea fadhila za kumzuru (kumtembelea) bibi Fatuma (a.s), miongoni mwa riwaya hizo ni:

  • 1- Kutoka kwa Saadi bun Saidi, kutoka kwa Abu Hassan Ridha (a.s) anasema: Nilimuuliza kuhusu kaburi la Fatuma bint Mussa bun Jafari (a.s) akasema: (Atakae mtembelea atapata pepo).
  • 2- Imamu Jawaad (a.s) anasema: (Atakae tembelea kaburi la shangazi yangu huko Qum atapata pepo).
  • 3- Kutoka kwa Saadi, kutoka kwa Imamu Ridha (a.s) anasema: Ewe Saadi kwenu kuna kaburi letu), nikamuambia! Kaburi la Fatuma bint Mussa? Akasema: (Ndio, Atakae litembelea akiwa anafahau haki yake atapata pepo).
  • 4- Imamu Swaadiq (a.s) anasema: (Hakika Mwenyezi Mungu ana haram, nayo ni Makka, na Mtume (s.a.w.w) ana haram, nayo ni Madina, na kiongozi wa waumini (a.s) ana haram, nayo ni Kufa, na sisi tuna haram, nayo ni mji wa Qum, atazikwa katika mji huo mwanamke miongoni mwa kizazi changu anaye itwa Fatuma, atakae mtembelea atapata pepo).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: