Kwa kutumia wataalamu wa kiiraq na baada ya kushindwa hospitali za kigeni kwa miaka 4: Hospitali ya Alkafeel yaondoa tatizo lililo kuwepo katika koo la kijana wa kiyemen…

Maoni katika picha
Siku baada ya siku hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kupata mafanikio katika sekta ya kutoa huduma kwa wagonjwa au katika sekta ya upasuaji, mafanikio hayo yameanza kufika hadi nje ya mipaka ya Iraq, na imekua kimbilio la wagonjwa wengi hasa wenye matatizo sugu, hali ya kijana wa kiyemen (s.m.m) ni moja miongoni mwa vielelezo vya mafanikio ya hospitali.

(s.m.m) ni kijana mwenye tatizo la koo, limeziba kwa kiasi cha asilimia 90, jambo linalo sababisha apumue kwa shida, alikua amesha enda katika hospitali nne, Yemen, Oman, Jodan pamoja na India, katika hospitali zote hizo hawakuweza kutatua tatizo lake, katika hatua ya mwisho na baada ya kupata ushauri kutoka kwa watu mbali mbali aliamua kuja Iraq katika hospitali ya rufaa Alkafeel, baada ya kuwasili kwake hospitalini, madaktari walimpokea na kuanza kumfanyia vipimo vya awali, jopo la madaktari wa kiiraq likiongozwa na daktari bingwa wa magonjwa ya pua, sikio na koo dokta Aadil Masudi waliamua kumfanyia upasuaji, dokta Masudi amebainisha kua: “Hakika jopo la madaktari chini ya usimamizi wetu limefanikiwa kumtibu kijana wa kiyemen mwenye umri wa miaka 28 aliye kua na tatizo la kuziba koo kwa asilimia 90 na kumfanya apumue kwa shida, tumemfanyia upasuaji wa kupanua koo na tumefanikiwa, upasuaji wa aina hii ni nadra sana kufanika, madaktari wengi walio baini tatizo lake hawakuweza kulitibu, kuanzia Yemen, India, Jodan na Oman”.

Akasema kua: “Hakika hali ya mgonjwa inaendelea vizuri, amesha anza kupumua kawaida na bado yupo chini ya uangalizi wa madaktari, tuna tarajia atarudi nchini kwao baada ya siku chache”.

Akaongeza kusema kua: “Hakika kijana huyu wa Yemen kuelekezwa na kushauriwa kwake aje katika hospitali ya rufaa Alkafeel ni dalili ya mafanikio ya kimatibabu yanayo patikana kwa wagonjwa”.

Kumbuka kua hospitali ya rufaa Alkafeel imesha fanya upasuaji mara nyingi tangu kuanzishwa kwake, tena katika maradhi ya aina mbalimbali, na asilimia kubwa ilifanikiwa, kutokana na vitu viwili vikuu: kwanza, umahiri wa madaktari wake wa kiiraq na wa kigeni, pili, uwepo wa vifaa tiba vya kisasa, pamoja na utukufu wa mwenye jina lililo pewa hospitali la Alkafeel ambaye ni Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zinazo tolewa na hospitali unaweza kuangalia katika mtandao wa hospitali: www.kh.iq au piga simu namba: 07602344444 au 07602329999.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: