Maahadi ya Qur’an tukufu asubuhi ya Juma Mosi (11.Rabiu-Thani 1439h) sawa na (30 Desemba 2017m) wamefanya hafla ya kuhitimu walimu wa kufundisha na kuhifadhisha Qur’an tukufu, hafla hiyo imefanyika ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Ataba tukufu.
Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu, kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, baada ya hapo ukafuatia ujumbe wa Maahadi ya Qur’an, ulio wasilishwa na mkuu wa Maahadi Shekh Jawaad Nasrawi, ambaye alisema kua, “Tangu kuanzishwa kwa Maahadi ya Qur’an tukufu, imechukua jukumu la kueneza utamaduni wa Qur’an kwa kufanya semina na nadwa katika sehemu mbalimbali hapa Iraq, pamoja na kusomesha namna ya kuhifadhi Qur’an tukufu, ratiba hizo zimekua za wazi kwa kila mtu kwa ajili ya kujenga uwezo wa kushiriki katika mashindano ya kitaifa na kimataifa, katika semina hii wameshiriki wasomaji wa Qur’an kutoka katika misikiti na Husseiniyya wapatao (200) na walimu kutoka mikoa ya: Bagdad, Karbala, Najafu, Diwaniyya, Baabil, Kuut na Naswiriyya”.
Akaongeza kusema kua: “Semina hii! Kwa utukufu wa viongozi wa Atabatu Abbasiyya na wakufunzi wa semina, imepata mafanikio makubwa, mafanikio haya pia yamesababishwa na nidhamu nzuri ya viongozi wa mradi huu, Maahadi ya Qur’an tukufu kupitia matawi yake yaliyopo nchi nzima inaendelea kutoa semina za Qur’an tukufu”.
Kisha ukafuatia ujumbe wa mkufunzi wa semina Dokta Raafii Aamiri, ambaye alisema kua: “Semina hizi zinachukuliwa kua ni muhimu sana na Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya, ni utukufu mkubwa kwangu kua mkufunzi wa semina hizi, ambazo zimedumu karibu mwaka na nusu, katika mikoa mbalimbali”.
Baada ya hapo ukafuata ujumbe wa washiriki ulio wasilishwa na Maitham Jaabir, ambaye alisema kua: “Tumepata utukufu mkubwa sana kushiriki katika semina ya Alkafeel awamu ya tatu ya walimu na mahafidhi wa Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya, semina zinazo endeshwa na Maahadi ya Qur’an tukufu, Mwenyezi Mungu ametuneemesha kwa kuhifadhi kitabu chake kitukufu na kuweza kukisoma kwa ufasaha, na sasa tunaweza kuisambaza elimu hii kwa watu wengine kama alivyo sema Mtume (s.a.w.w) (Mbora wenu ni yule atakae jifundisha Qur’an na akaifundisha), tunatoa shukrani nyingi kwa kila aliye changia kufanikiwa kwa semina hizi za Qur’an tukufu, na tunatamani ziendelee kufanyika katika mikoa yote ya Iraq ili faida hii iwafikie watu wengi zaidi”.
Hafla ilikua na mahudhurio makubwa, kiongozi wa wakfu shia wa zamani Sayyid Swaaleh Haidari pia alihudhuria, pamoja na viongozi wengi wa Ataba tukufu, vilevile ilionyeshwa filamu inayo elezea utendaji wa mradi huu kuanzia mwanzo wa mradi hadi mwisho, na mwisho kabisa wa hafla washiriki wa semina wakapewa vyeti.