Kikosi cha wapiganaji cha Abbasi chafanya kongamano la kusherehekea ushondi na chatumia wito wa Marjaa kama kauli mbiu yake..

Maoni katika picha
Chini ya kauli mbiu isemayo (Ushindi wetu ni matokeo ya mwitikio wa wairaq) na chini ya usimamizi wa waziri mkuu Dokta Haidari Abadi, kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) asubuhi ya Juma Mosi (11 Rabiu-Thani 1439h) sawa na (30 Desemba 2017m) kimefanya kongamano la kusherehelea ushindi katika ukumbi wa Hakim ndani ya chuo kikuu cha Bagdad.

Kongamano limepata mahudhurio makubwa, yaliyo ongozwa na waziri mkuu Dokta Haidari Abadi, kamanda wa kikosi cha kupambana na ugaidi, waziri wa elimu ya juu, mshauri wa mambo ya kitaifa, rais wa vikundi vya Hashdi Sha’abi na kundi kubwa la wapiganaji wa kujitolea wa kikosi cha Abbasi.

Baada ya kuimbwa wimbo wa taifa kama ishara ya kuanza kwa kongamano, lilifunguliwa rasmi kwa Qur’an tukufu na ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, kisha likafuata tamko la makaribisho lililo tolewa na ustadh Maitham Zaidi, kiongozi mkuu wa kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s), miongone mwa aliyo sema ni:

“Tuna utukufu mkubwa leo kua pamoja na nyie katika kusherehekea ushindi ulio patikana kutoka na damu za wairaq na kupigana kwao jihadi, kuna wanao sema nyie mara nyingi mnakariri neno (ushindi wa Iraq), tunawaambia; katika khutuba ya ushindi Mheshimiwa Marjaa dini mkuu Sayyid Ali Sistani alitaja neno hilo na yanayo fanana na hilo mara kumi na moja, ni haki ya kila mtu duniaji kujifaharisha kwa taifa lake, mji wake, turathi zake na utamaduni wake, na sisi hatuamini kama kuna nchi tukufu zaidi ya nchi yetu, Iraq inahistoria ndefu ya mwanadamu, sisi ndio tulio fundisha ulimwengu uandishi wa sheria, wairaq ndio walio wafundisha walimwengu namna ya kujitambulisha kwa maandishi, katika ardhi yetu wameletwa Mitume wengi, Mawaliy na waja wema, na sasa hivi mmeona namna wairaq walivyo weka rekodi ya ushujaa kupitia damu za mashahidi wao, walipo pigana kijasiri na magaidi wa Daesh, ambao hawakuilenga Iraq kama hitimisho la vita yao, bali walitaka kutumia Iraq kama njia ya kufikia mataifa mengine, kwa utukufu wa damu za mashahidi tumeweza kuwamaliza madaesh na kukomboa ardhi yote”.

Akaongeza kusema kua: “Fatwa tukufu ilikua ponyo kwa majeraha ya Iraq, iliwarudisha wairaq katika ujasiri wao, na leo tupo katika hatua mpya ya ujenzi, tuta acha kambi za jeshi kwa kuweka siraha chini na kushikamana mkono kwa mkono na kupambana na ufisadi, ufisadi ni tatizo kubwa lisilo takia mema taifa letu, ufisadi ukiendelea utaharibu mafanikio yetu dhidi ya daesh, kwani ndio sababu kubwa iliyo sababisha Daesh kuingia hapa Iraq”.

Akabainisha kua: “Kikosi cha wapiganaji cha Abbasi kinazingatia sana fatwa tukufu ya Marjaa dini mkuu Sayyid Sistani, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, Hashdi Sha’abi itakua na nafasi kubwa katika hatua ifuatayo, sio kwa kuingia katika uchaguzi moja kwa moja, bali katika ujenzi wa taifa, na wala hakuna chama chenye jina la Hashdi Sha’abi lakini tutasaidia mchakato wa uchaguzi”.

Baada yake ulifuata ujumbe wa waziri mkuu Dokta Haidari Abadi, ambaye alianza kwa kupongeza ushindi wa wairaq kwa kusema: “Tunapongeza sana ushindi huu mkubwa kwa mara nyingine, tunawapongeza kwa kua na mwaka wa ushini na sasa tunaingia katika mwaka mpya bila kua na Daesh, ushindi huu umetokana na umoja wa raia wetu, na umeletwa na wapiganaji wetu watukufu, mashujaa na damu tukufu za mashahidi na kutokana na mihanga ya majeruhi na mtu yeyote aliye changia kitu chochote au akatumia muda wake, tuna pongeza sana na kusifu fatwa tukufu iliyo tolewa na Marjaa dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ali Sistani, fatwa ambayo iliitikiwa na watu wote wa Iraq, na ikaleta mafanikio makubwa, hakika raia walipigana kwa pamoja kuhami taifa lao na maeneo matukufu, na wao ndio walio leta ushindi huu, ushindi ulipatikana pale wapiganaji wa kujitolea (Hashdi Sha’abi) walipo simama pamoja na jeshi la serikali, tunapongeza pale walipo simama kikosi cha kupambana na ugaidi pamoja na serikali, hali kadhalika walipo simama wapiganaji wa kikoo, hasa walipo simama vikundi vyote vya wapiganaji pamoja na Bashmerka katika vita ya kukomboa mji wa Mosul na wakafanikiwa kuukomboa mji mzima wa Nainawa, hakika wapiganaji walisaidiana bega kwa bega kutafuta ushindi huu, watu hawa tuna deni kwao, hatupaswi kuwasahau mashahidi na kila aliye jitolea kwa namna moja au nyingine, lazima tuwakumbuke daima, ni kweli kua serikali ina jukumu la kwanza la kuwakumbuka watu hawa lakini pia ni jukumu la kijamii, tuwatafute na tuwasaidie watoto wa mashahidi, familia za mashahidi, majeruhi, walio pata ulemavu, natoa wito kwa wahisani na raia kwa ujumla kila anaye weza aunde taasisi au kikundi kwa ajili ya kusaidia makundi haya niliyo taja, na serikali ipo pamoja na nyie, hii ni sehemu ndogo tunayo weza kuwafanyia familia za mashahidi na majeruhi, na kulinda ushindi mtukufu ulio patikana kutokana na juhudi za wairaq wenyewe”.

Akaendelea kusema kua: “Kuna watu wanataka tupoteze ushindi huu kwa mambo yao, tunapo sema watu wa kusini, wa kati na kaskazini, wote walitoka kwenda kuwanusuru ndugu zao katika miji mingine, wakapigana kishujaa bila kujali mlengo wa kisiasa, kichama wala kikabila au kundi fulani, bali walipigana kwa ajili ya kuhami taifa lao na maeneo matukufu, haifai kutumia kujitolea kwao kwa maslahi binafsi, jambo la kusikitisha kuna baadhi ya watu wanapaza sauti zao na kuongea mambo ya ajabu yasiyo faa kabisa”.

Waziri mkuu akaongeza kusema kua: “Tunapo taja familia tukufu za watu walio kimbia miji yao baada ya kuvamiwa na Daesh, na tunapo taka kuwarudisha katika miji yao, pia kuna watu wanajitokeza hapa na pale na kuongea mambo mabaya, wanataka kuendelea kutengeneza matatizo, baadhi ya watu hao ndio walio wafungulia milango madaesh, walikua wakijifaharisha kwa kuwepo daesh, hatusahau na wala hapasi kusahau, walikua wanasema Daesh wamekuja kuwakomboa, lakini wakombozi wao waliwapiga na kuwaua hadi wakakimbia nyumba zao, hali kadhalika haitakiwi kusahau mafisadi walio pora mali za serikali kwa maslahi ya Daesh, Daesh wasinge weza kuingia mkoa baada ya mkoa kama sio kusaidiwa na genge hili la mafisadi”.

Hafla ilihitimishwa kwa mashairi yaliyo imbwa na wahusika wa ushindi huu ulio patikana kwa mshikamano wa wairaq, walipo simama safu moja kuitikia mito wa Marjaa wa fatwa tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: