Mkuu wa kituo cha nakala kale katika wakfu wa kisunni Dokta Abdurazaaq Ahmadi Harbi amesisitiza kua: “Tupo tayali kushirikiana na Atabatu Abbasiyya tukufu katika sekta hii (turathi za umma), na tumekusudia kuboresha ushirikiano na kufanya kazi kwa pamoja katika sekta ya kutunza nakala kale kwani zinawakilisha turathi za umma”.
Akaongeza kusema kua: “Tunafanya juhudi ya kudumisha uhusiano na kituo cha kukarabati nakala kale cha Atabatu Abbasiyya tukufu. Hakiha kituo hicho kina maendeleo makubwa, tunapata uzowefu kutoka kwa watumishi wao, kwani wao wana ujuzi makubwa, sisi tumeanza kazi katika kituo cha nakala kale za wakfu wa kisunni kabla ya miaka miwili, wakati kituo cha nakala kale cha Atabatu Abbasiyya kimeanza kazi miaka mingi iliyo pita, na wamesha pata uzowefu mkubwa, hivyo sisi tunasoma kutoka kwao na tunajifunza uzowefu wao ambao sisi bado hatujapata hadi sasa”.
Aliyasema hayo Dokta Abdurazaaq Ahmadi Harbi alipo tembelea kituo cha kukarabati nakala kale cha Atabatu Abbasiyya tukufu, ambaye pia alikua msimamizi wa semina ya kukarabati nakala kale waliyo pewa watumishi wa kituo cha nakala kale cha wakfu sunni kwa muda wa siku kumi.
Mwishoni mwa ziara yake iliyo husisha kutembelea sehemu za kituo hiki Harbi alisema kua “Hakika ni utukufu mkubwa kwetu, kutembelea sehemu hii takatifu, na furaha kubwa sana kukutana na ndugu zetu na marafiki wetu wapenzi katika mji huu mtukufu, na kupata fursa ya kuangalia mafanikio makubwa yaliyo fikiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika sekta ya kukarabati nakala kale na kurejesha thamani na uhai wa lulu za historia ya umma”.
Akaongeza kusema kua: “Ni aibu kubwa kwetu, babu zetu kituachia kitu kizima hafafu kiharibikie mikononi mwetu, mradi huu ni muhimu sana kwa sababu tunatekeleza wajibu wetu wa kuhakikisha tunaukabidhi umma turathi salama kama zilivyo achwa na babu zetu”.