Muendelezo wa mafanikio yake: Skaut ya Alkafeel yafanya shindano la mwaka wa tatu…

Maoni katika picha
Skaut ya Alkafeel ambayo ipo chini ya idara ya watoto na makuzi katika Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya shindano la mwaka wa tatu, ambalo ni sehemu ya kukamilisha mafanikio ya awamu zilizo pita, na kufungua hatua mpya ya mashindano yajayo yanayo lenga kukuza akili za watoto na kuendeleza vipaji vyao pamoja na kuchangamsha akili zao katika masomo na kuwafanya waweze kushindana kimasomo na hatimae wawe na viwango vya juu katika elimu.

Na hili ndio lengo kubwa la Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha habari na utamaduni hasa idara na watoto na makuzi, kutumia njia hii nzuri na muhimu katika kufikisha mafunzo yanayo fungamana na Qur’an tukufu pamoja na Ahlulbait (a.s), kadhalika baadhi ya mafundisho ya kimaadili yanayo saidia kujenga mustakbali wa mtu na kujenga taifa letu na jamii kwa ujumla.

Mashindano ya Alkafeel ya kila mwaka yanalenga watoto wenye umri wa miaka (9 hadi 17) miongoni mwa wanafunzi, sifa pekee ya mashindano haya ni kwamba yanahusisha sekta ya dini, yanalenga kuwaendeleza kifiqhi na masomo mengine ya dini, mashindano ya mwaka huu yamehusisha mada kumi, ambazo ni: Qur’an na ulezi wa nyoyo, Ashura, Aqida yangu, Fiqhi ndogo, Ahlulbait (a.s), kisa na hekima, uchoraji wa ramani, wasubiriaji, fikiri pamoja nami, barua na amana. Kila mada inamaswali kadhaa.

Katika mashindano haya zimeshiriki shule za Karbala tukufu na mikoa mingine, kama vile Najafu na Diwaniyya, mwaka huu zimeshiriki shule zaidi ya 35, na zimeandikwa jumla ya karatasi za maswali 5000 na kutawanywa katika shule hizo, pamoja na kuelezea malengo na madhumini ya shindano hili, zitakusanywa na kusahihishwa na kamati maalumu iliyo pewa jukumu hilo.

Zimeandaliwa zawadi (250) za watakao faulu katika shindano hili, zinazo endana na umri wa washiriki, (50) katika zawadi hizo ni Baskeli, na kutakua na hema maalumu la Skaut kwa ajili ya kupumzika kwa wototo (100) watakao faulu, na (100) wengine watapewa zawadi za vitu kutoka katika idara ya watoto na makuzi.

Kumbuka kua wazo la kuanzishwa kwa mashindano haya lilipatikana katika mwezi wa Muharam mwaka 1436 hijiriyya, na lilitokana na maadhimisho ya Imamu Hussein kwa wanafunzi wa shule za Karbala, na ziliandaliwa zawadi kwa ajili wa kuvutia wanafunzi ili washiriki katika shindano hilo, idadi ya washiriki ilikua zaidi ya wanafunzi 2500 kutoka vitongoji vya mkoa mtukufu wa Karbala, baada ya hapo lilifanyika kongamano la kutumia kura kuwapata washindi, baada ya kuonekana mafanikio, ndipo jambo hili likaingizwa katika jumuiya ili kulifanya kua endelevu na lifanyike kila mwaka, ndipo yakafanyika marekebisho katika uandaaji wa maswali na utoaji wa zawadi pamoja na mpangilio wote kwa ujumla.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: