Atabatu Abbasiyya tukufu jirani na malalo ya kiongozi wa waumini yawapa zawadi familia za mashahidi waliokua wanafunzi wa hauza…

Maoni katika picha
Katika mfululizo wa ratiba yake ya kusaidia familia za mashahidi wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi, iliyo anza toka kutoliwa fatwa tukufu ya jihadi ya kujilinda, Atabatu Abbasiyya tukufu yatoa zawadi kwa familia za mashahidi waliokua wanafunzi wa hauza katika mji mtukufu wa Najafu, mashahidi ambao walijitolea damu zao kwa ajili ya kukomboa ardhi kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh, na walikua na mchango mkubwa sana katika kufanikisha ushindi huu, wakati mwingine walifanya kazi kama wazazi waelekezaji kwa wapiganaji, na wakati mwingine walikua kama walimu, wakati mwingine walikua sawa na marafiki wema, pia walikua sawa na waokozi, pia wakati mwingine walikua sawa na wanafunzi, na walifanya kazi vilevile kama watoa huduma kwa wapiganaji na wakati mwingine walishika siraha na kua wapiganaji watiifu, hadi likapatikana kundi kubwa la mashahidi miongoni mwao.

Hafla hii imefanywa kwa kushirikiana na Atabatu Alawiyya tukufu, katika msikiti wa Khadhraa na kuhudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i) na kiongozi wa serikali wa mji wa Najafu pamoja na jopo la viongozi wa hauza tukufu, na wanafamilia za mashahidi na wawakilishi wa Ataba tukufu pamoja na jopo la viongozi wa wapiganaji wa Hashdi Sha’abi.

Baada ya Qur’an tukufu na kusoma surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, ulifuata ujumbe wa kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, ambaye alisifu namna wanajeshi na Hashdi Sha’abi walivyo jitolea katika mapambano hususan mashahidi waliokua wanafunzi wa hauza, na akasisitiza umuhimu wa kuendelea kuzisaidia familia za mashahidi walio jitolea kila walicho nacho kwa ajili ya kuilinda Iraq na maeneo matukufu”.

Baada ya hapo Sayyid Adnani Mussawi kutoka katika kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu aliwakumbuka majemedali hawa kupitia beti za maombolezo.

Naye rais wa kitengo cha dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, Shekh Swalahu Karbalai alibainisha kua: “Kutoa zawadi kwa familia za mashahidi katika eneo hili la malalo ya kiongozi wa waumini (a.s), ni sehemu ya muendelezo wa mradi huu ulio anza tangu kutolewa kwa fatwa tukufu ya jihadi ya kujilinda, na bado tunaendelea sambamba na kuendelea kusisitizwa na Marjaa dini mkuu kuhusu umuhimu wa kuzisaidia familia za mashahidi katika kila hali, hafla hii inayo fanyika katika malalo ya kiongozi wa waumini (a.s) kwa kushirikiana na Atabatu Alawiyya tukufu, kwa kutoa zawadi kwa familia (70) za mashahidi waliokua wanafunzi wa hauza, na tunaendelea na ratiba hii hadi tuzifikie familia zote za mashahidi watukufu”.

Kumbuka kua Marjaa dini mkuu amehimiza mara nyingi umuhimu wa kuzijali na kuzisaidia familia za mashahidi, hivi karibuni kasisitiza hilo katika khutuba ya ushindi, pale alipo sema: “Hakika mashahidi wema walio lowanisha udongo wa Iraq kwa damu zao tukufu, wamekwenda katika maisha ya milele wakiwa wameloa damu, hakika ni utukufu wetu sote, wapo sehemu tukufu mno mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu, jambo dogo sana miongoni mwa wajibu wetu kwao, ni kuzisaidia familia zao, wajane, mayatima na wengineo, hakika kuwatunza watu hao kwa kuwapa mahitaji muhimu katika maisha yao, kama vile; makazi, afya, elimu, na matumizi madogo madogo wanayo hitaji katika maisha ya kila siku ni jukumu la kiuzalendo na ki-akhlaq, pia ni wajibu wetu sote, hautafanikiwa umma usiojali familia za mashahidi wao walio jitolea maisha kwa ajili yao, jukumu hili kwanza ni la serikali kuu na bunge, wanatakiwa watenge kiasi cha pesa kwa ajili ya kusaidia familia za mashahidi hususan walio pata shahada dhidi ya magaidi wa Daesh, jambo hilo linatakiwa kupewa kipawa mbele zaidi kuliko mambo mengine”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: