Miongoni mwa bidhaa za shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud, waja na jibu sahihi la kurutubisha mazao na kuongeza uzalishaji…

Maoni katika picha
Miongoni mwa mfululizo wa utengenezaji wa bidhaa za mbolea unaofanywa na shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wametoa bidhaa mpya ya (Sanaabil Dhahabiyya), ambayo ni miongoni mwa mbolea za maji zenye ubora mkubwa zinazo kidhi haja ya wakulima.

Mbolea hii ni miongoni mwa mbolea zenye uwezo mkubwa wa kurutubisha mimea na kuongeza mavuno, ubora wake umethibitika katika miaka ya hivi karibuni kwa ushuhuda wa wakulima wenyewe, pamoja na kuongeza mavuno, pia ina kila sifa ya ubora wa mbolea za kisasa, pia watumiaji wake wamethibitisha kua haina sumu.

Sanaabil Dhahabiyya imetengenezwa rasmi kwa ajili ya kukuzia mimea, na inachukuliwa kua suhulisho la matatizo mengi ya ukuaji wa mimea, inasifiwa kwa:

  • 1- Inanyonywa kwa urahisi na mimea.
  • 2- Inaifanya mimea (hususan ngano) kua na uwezo mkubwa wa kuvumilia mazingira magumu ya kuongezeka na kupungua kwa viwango vya joto na ubaya wa maji au udongo.
  • 3- Ina nafasi kubwa ya kuongeza mavuno.
  • 4- Ina nafasi kubwa ya kulinda mimea isishambuliwe na wadudu au magonjwa.

Sanaabil Dhahabiyya imetengenezwa na vitu vingi, uchafu wa baharini, asidi ya amino pamoja na virutubishi lishe na aina nyingine ya virutubishi vidogo na vikubwa ambavyo hutumiwa na mimea ya aina zote.

Matumizi yake ni; lita (5) unaweza kuipulizia katika shama la dunam (4) (Heka mbili takriban) za ngano, shairi na mimea mingine, unaweza kutumia vifaa vya kisasa katika kupulizia mbolea hii.

Kumbuka kua bidhaa hii inapatikana katika vituo vya mauzo vya shirika hili vilivyopo ndani na nje ya mkoa wa Karbala, kwa maelezo zaidi unaweza kupiga namba zifuatazo (07801930125 au 07801035422) au fika moja kwa moja katika ofisi za shirika zilizopo katika barabara ya Karbala – Najafu mkabala na nguzo namba 1145.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: