Atabatu Abbasiyya tukufu yashiriki katika maonyesho ya kimataifa ya vitabu katika chuo kikuu cha Hilla, na mkuu wa chuo asifu ushiriki wao na asema umependezesha maonyesho…

Dokta Hassan Masudi akifungua moja ya kitabu katik
Mkuu wa chuo kikuu cha Hilla Dokta Hassan Masudi amesema kua ushiriki wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa ya kwanza yanayo simamiwa na kituo cha elimu, umependezesha maonyesho hayo kutokana na vitu wanavyo vionyesha, kufuatia mafanikio makubwa waliyo nayo yanayo endana na makusudio ya maonyesho haya, ambayo ni sehemu ya mafanikio ya kielimu, tunafanya juhudi za kuimarisha ushirikiano wetu na kufanya miradi mingine katika siku zijazo.

Akaongeza kua: “Miongoni mwa mikakati ya chuo chetu ni kufungua ushirikiano na taasisi za kielimu pamoja na Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya), na ushiriki wao katika maonyesho haya ni dalili ya muendelezo wa mchakato huo, tumeona tawi la Atabatu Abbasiyya lina mwitikio mkubwa, wanaonyesha vitu nadra na vinavyo burudisha roho, tunaona bashasha usoni kwa kila mtu anaye tembelea tawi hili, tuna ishukuru sana Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kukubali mwaliko wetu wa kuja kushiriki katika maonyesho haya, na shukrani za pekee ziwaendee wahudumu wake wote, tunatarajia kuendea kushirikiana zaidi katika kuwatumikia raia wa Iraq.

Yalitokea hayo wakati mkuu wa chuo Dokta Hassan Masudi alipo tembelea tawi (banda) la Atabatu Abbasiyya katika shughuli ya ufunguzi wa maonyesho hayo iliyo fanyika asubuhi ya Juma Nne (14 Rabiu-Thani 1439h) sawa na (02 Januari 2018m), katika maonyesho haya, zimeshiriki asasi za kitaifa na kimataifa, chini ya kauli mbiu isemayo (Utamaduni wa Karatasi).

Katika maonyesho haya; Atabatu Abbasiyya tukufu imewakilishwa na kitengo cha habari na utamaduni na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu, wameonyesha vitu mbalimbali miongoni mwa bidhaa zao katika sekta ya kibinadamu na kielimu, vitabu, majarida pamoja na machapisho ya dini na picha mbalimbali.

Kumbuka kua ushiriki huu ni miongoni mwa mikakati ya Atabatu Abbasiyya tukufu ya kujenga ushirikiano na taasisi za elimu hapa Iraq, zinazo endana na malengo yao, ya kukuza elimu na uwezo wa wanafunzi wa vyuo, hakika Atabatu Abbasiyya imesha shiriki mara nyingi katika maonyesho na makongamano ndani na nje ya nchi, na miongoni mwake ni maonyesho haya, ushiriki huu unasaidia kuijulisha jamii mafanikio na maendeleo yaliyo fikiwa kielimu na kiujenzi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: