Kuanza hatua ya kwanza ya mradi wa kuweka dhahabu katika ukuta wa sehemu ya dhahabu wa kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s)…

Mchoro wa mradi
Kutokana na mchoro ulio andaliwa na wahandisi wanao tekeleza sehemu ya kwanza ya hatua ya pili katika mradi wa kuimarisha ukuta na kurejeshea dhahabu katika sehemu kubwa yenye dhahabu inayo julikana kama (Twarima) katika kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s), ambapo kazi ya kuondoa vifuniko vya zamani kwa ajili ya kuanza hatua ya pili inayo husisha kukarabati ukuta na kuuandaa kwa ajili ya kuambatanishwa na ukuta wa pili, utakao unganishwa na ukuta wa zamani kiutalamu kwa kutumia vifaa maalumu vinavyo kubali kuvishwa vifuniko vipya vya dhahabu, vifuniko hivyo vimesha anza kutengenezwa kwa kutumia dhahabu na mina chini ya kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh alipo ongea na mtandao wa Alkafeel alisema kua: “Sehemu ya kwanza ya mradi huu ni muhimu sana kwa sababu sehemu zote zijazo zinaitegemea, na inatekelezwa kwa kufuata mchoro ulioandaliwa na kitengo chetu na kwa kufuata usanifu ulio fanywa kwa ajili ya mradi huu, na shirika linalo tekeleza mradi ni shirika la ujenzi la Ardhi tukufu, wamejipanga kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa mradi huu ndani ya muda ulio pangwa”.

Akabainisha kua: “Sehemu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi huu, imehusisha kutengeneza vitendea kazi maalumu, vitakavyo saidia kutokatisha harakati za mazuwaru wakati wa utekelezaji wa mradi, na kuweka namba katika vifuniko vya zamani, na kuvikusanya katika masanduku maalumu kisha kuyakabidhi katika kitengo cha zawadi na nadhiri, kwa ajili ya kuvitumia katika miradi mingine, baada yapo ukuta umesafishwa vizuri na kurekebisha sehemu zilizokua zimeharibika, na kuhakikisha umekua imara kila sehemu, kwa kumaliza kazi hizi, ukuta utakua tayali kwa hatua nyingine ya kuambatanishwa na ukuta mpya wa kisasa ulio tengenezwa kwa ustadi na ubora wa hali ya juu ambapo hatua hiyo tutaianza hivi karibuni”.

Kumbuka kua sehemu hii ya mradi inakamilisha hatua zilizo tangulia na itapendezesha muonekano wa Atabatu Abbasiyya tukufu, pia itapendezesha muonekano wa majengo ya Karbala, unao endelea kujengwa kila siku kiutaalamu na umaridadi mkubwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: