Chuo kikuu cha Ameed chafanya nadwa kuhusu athari za dawa za kulevya na namna ya kupambana nazo…

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kupitia kitivo cha uuguzi, kinaendesha nadwa (darasa mjadala) kuhusu dawa za kulevya na athari zake katika jamii na kiafya pamoja na kuangalia njia za kupambana nazo, chini ya kauli mbiu isemayo (Hatari za dawa za kulevya katika maisha ya mwanadamu) kwa kusaidiana na ofisi ya kupambana na dawa za kulevya za mkoa mtukufu wa Karbala.

Nadwa imefanyika katika ukumbi wa kitivo cha uuguzi na kuhudhuriwa na rais wa chuo na idadi kadhaa ya walimu pamoja na wanafunzi wa chuo, pamoja na wawakilishi kutoka katika sekta zingine.

Nadwa ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu, halafu ukafuatia ujumbe wa rais wa chuo cha Ameed Dokta Jaasim Marzuki, alizungumzia madhara ya dawa za kulevya na athari zake katika jamii, na imekua ni moja ya hatari kubwa katika jamii, akatoa wito wa kuongeza juhudi katika kupambana na hatari hii inayo ingia katika jamii za wairaq.

Katika nadwa hii zilitolewa mada mbalimbali, mlango wa kuwasilisha mada ulifunguliwa na naibu mkuu wa taaluma wa kitivo cha uuguzi Dokta Ridha Twaai, mada yake ilihusu madhara ya dawa za kulevya kiafya, kwa mtu anaye tumia dawa hizo, na akafafanua aina za magonjwa yanayo sababishwa na kutumia dawa za kulevya, ikafuatia mada ya naibu wa mkuu wa ofosi ya kupambana na dawa za kulevya Hassan Jaazi, katika mkoa wa Karbala, alizungumzia aina mbalimbali za dawa za kulevya zinazo tumika zaidi, na ambazo zimekua hatari kubwa kwa nguvu kazi ya taifa, kwani zinatumiwa na watu wa rika zote hadi wanawake.

Mada ya mwisho ilitolewa na mwalimu msaidizi Ahmadi Yaquub, ambaye ni mkuu wa idara ya sheria katika chuo kikuu cha Ameed, alizungumzia vipengele vya sheria vinavyo tumiwa na mahakama katika kutoa adhabu kwa wahusika wa dawa za kulevya, ambapo kuna kifungo hadi cha maisha, kunyongwa pamoja na kulipa faini ya pesa.

Sehemu ya mwisho ya nadwa ulikua mjadala huru kwa wanafunzi wa chuo, na wakauliza maswali kwa watoa mada kuhusu hatari za dawa za kulevya inayo tishia kundi la vijana kwa kiasi kikubwa katika jamii, kutokana na dawa hizo kusambaa katika miji mingi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: