Awamu ya kumi na nne: Kamati ya maandalizi ya kongamano la Rabiu Shahada yaanza kufanya vikao na yaufanya ushindi wa Iraq dhidi ya magaidi kua kauli mbiu ya kongamano…

Sehemu ya kongamano
Kamati ya maandalizi ya kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada yaanza kufanya vikao kwa ajili ya kujiandaa na awamu ya kumi na nne ya kongamano hilo ambao husimamiwa na uongozi mkuu wa Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya), hufanywa sambamba na kumbukumbu ya kuzaliwa kwa nuru za Muhammad (a.s) katika mwezi wa Shabani, kuanzia mwezi tatu hadi mwezi saba.

Makamo rais wa kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya Sayyid Aqiil Yaasiri ametuambia kuhusu vikao hivyo kua: “Kongamano la Rabiu Shahada ni tukio muhimu sana linalo fanjwa na kusimamiwa na uongozi mkuu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kwa ajili ya kulinda mafanikio mazuri yaliyo patikana katika makongamano yaliyo pita, na kuhakikisha kongamano hili linakua zuri, kamati ya maandalizi imeanza kufanya vikao, na vitaendelea kufanywa kila wiki hadi siku ya kuanza kongamano, fahamu kua kongamano hili limekua alama kubwa ya kiutamaduni duniani linalo pigiwa mfano, na sauti yake inafika kila kona ya dunia”.

Akaongeza kusema kua: “Awamu ya kumi na nne ya kongamano hili itakua ya aina yake, kwani Iraq inasherehekea ushindi dhidi ya magaidi wa Daesh, kamati ya maandalizi imechagua kauli mbiu ya mwaka huu kua ni (Tumepigana kutokana na Hussein (a.s) na tumeshinda kutokana na fatwa), kamati kuu ya maandalizi imeteua viongozi na wajumbe wa kila idara pamoja na kugawa majukumu, nayo pia itakua na vikao vya mara kwa mara, yote haya ni kwa ajili ya kuhakikisha kongamano linafanyika kwa ufanisi na umaridadi mkubwa, na kuhakikisha faida kubwa inapatikana, pia kulifanya liendane na hadhi na heshima ya Ataba mbili tukufu”.

Kumbuka kua kongamano la kitamaduni na kimataifa Rabiu Shahada, linalo andaliwa na kusimamiwa na uongozi mkuu wa Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) kila mwaka, kwa ajili ya kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa wajukuu wa Mtume (s.a.w.w), Imamu Hussein, ndugu yake Abulfadhil Abbasi na Imamu Sajjaad (a.s), hufanywa kila mwaka, ni moja ya harakati zinazo lenga kutoa elimu kwa jamii na kuongeza uwelewa wa dini kwa ujumla, pamoja na kubainisha athari na faida za muhanga wa Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: