Kufuatia juhudi za kuboresha kilimo Iraq, shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa latengeneza mbolea ya maji yenye ubora mara mbili…

Maoni katika picha
Sehemu kubwa ya ardhi ya Iraq inamatatizo makubwa, kuna sehemu zinamatatizo ya maji ya kumwagilizia na sehemu zingine zina matatizo ya ardhi yenyewe, pia kuna matatizo ya maradhi ya mimea na uwepo wa mbolea isiyo faa kumesababisha kuharibika kwa udongo ulio kua na rutuba ya kustawisha miti ya matunda na mimea mingine.

Shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud, daima limekua likitafuta ufumbuzi wa matatizo ya kilimo, mara hii wametengeneza mbolea ya maji yenye ubora mara mbili, na yenye mafanikio makubwa katika kukuza mimiea, inarutubisha mimea kwa haraka.

Mbolea hii inarutubisha mimea na kuifanya ikuwe kwa haraka, huku ikiikinga kutokana na maradhi mbalimbali, na kuiwezesha kuhimili mazingira tofauti, kama vile mabadiliko ya hali ya hewa, ubaya wa maji ya kumwagilizia, pia mbolea hii inaongeza upambaji wa mimea na kurefusha muda wa mavuno, ubora mwingine wa mbolea hii, inafyonzwa kwa urahisi na mimea, na inafaa kutumiwa katika aina zote za mimea.

Mbolea hii ni miongoni mwa bidhaa zinazo zalishwa na kiwanda hiki, na zipo za aina tofauti kulingana na mahitaji ya watumiaji, pia shirika limesha toa maelekezo kamili kuhusu namna ya kuitumia, na kuhakikisha inafanya mapinduzi ya uzalishaji wa mimea kwa kiwango kikubwa.

Kumbuka kua mbolea hii inapatikana katika vituo vya mauzo ya moja kwa moja ya shirika hili ndani na nje ya mkoa wa Karbala, kwa maelezo zaidi piga simu namba: (07801930125 au 07801035422), au unaweza kutembelea moja kwa moja kituo cha shirika kilichopo katika barabara ya Karbala – Najafu mkabala na nguzo namba (1145).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: