Kwa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya tukufu, uongozi wa bustani za kupumzikia katika mji wa Baabil wafanya nadwa (darasa mjadala) kuhusu changamoto za umoja…

Maoni katika picha
Kwa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya tukufu, uongozi wa bustani za kupumzikia katika mkoa wa Baabil, wamefanya nadwa kuhusu changamoto zinazo ukabili umoja, mtoa mada alikua ni Dokta Shaamil Muhsin Haadi, mwakilishi wa Atabatu Abbasiyya katika bara la Marekani ya kaskazini, nadwa hiyo wamefanyia katika eneo la bustani ya kupumzikia iliyopo mjini Hilla, kwa lengo la kuongeza uwelewa kuhusu changamoto za umoja.

Nadwa ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu, kisha ikasomwa surat Fat-ha, kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, walio jitolea damu zao takatifu, halafu likafuatia shairi lililosomwa na mshairi maarufu bwana Dhiyaau Abadi kuhusu ushindi wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi dhidi ya magaidi wa Daesh.

Baada ya hapo Dokta Shaamil Muhsin Haadi akatoa muhadhara kuhusu changamoto za umoja, na namna ya kuamiliana na waathirika wa kunyanyapaliwa jambo ambalo limeenea katika jamii, takwimu zinaonyesha idadi ya watu wanao kumbwa na tatizo la kunyanyapiliwa inaongezeka na wala hakuna juhudi zinazo fanywa na serikali kwa ajili ya kupambana na tatizo hili, muhadhara ulikua na nafasi ya maswali na majibu kutoka kwa wahudhuriaji, ambao wengi wao walikua na watoto walio wahi kukumbwa na tatizo la kubaguliwa.

Ustadh Abdul-Amiri Awidi mmoja wa viongozi wa waangalizi wa bustani za kupumzikia, aliongea kuhusu mada ya nadwa, huku Dokta Shaamil Hadi akizungumzia mambo muhimu kuhusu “Changamoto zinazo tishia umoja na sababu zake pamoja na njia ya kuzitatua changamoto hizo zinazo onekana leo hii katika jami yetu, hii ni nadwa ya wazi, inayo husu wazazi wenye watoto wanao kubwa na tatizo la kubaguliwa, na vituo vinavyo angazia tatizo hili ni vichache sana hapa Iraq, katika mkoa wa Baabil na mikoa ya jirani hakuna kituo chochote kunacho jishughulisha na tatizo hili zaidi ya Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya), na kuna matukio mengi ya vitendo vya ubaguzi, na sisi leo hii tunaumuhimu mkubwa wa kujenga maelewano, na tunatamani kuona serikali inalipa umihimu swala hili linalo gusa jamii ya wairaq”.

Mwisho wa nadwa, uongozi wa wasimamizi wa bustani za kupumzikia walitoa shukrani nyingi kwa viongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na kila mtu aliye shiriki katika nadwa hii, sambamba na kutoa zawadi kidogo, waliiomba jamii ifuate nyayo za Atabatu Abbasiyya tukufu za kujenga maelewano na tabaka zote za watu katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: