Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi chini ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, wanajenga ukumbi kwa ajili ya kuadhimishia matukio ya kidini pamoja na vyoo katika mazaru ya Sayyid Habibu bun Sayyid Ibrahim Almujaab, pamoja na mazaru ya dada yake Alawiyya (a.s) katika mkoa wa Diwaniyya wilaya ya Twaliah, ujenzi huu unafanywa kutokana na maombi rasmi kutoka katika idara ya mazaru tukufu, yaliyo wasilishwa katika ofisi za Atabatu Abbasiyya na kukubaliwa kwa maombi hayo.
Mafundi walianza kutekeleza mradi kwa muda ulio pangwa, wamejenga ukumbi wa kuadhimishia matukio ya kidini wenye ukubwa wa 2m300 na upana wa (12*25) na urefu wa mt. 3.6, kwa kutumia tharmastun na chuma, huku paa lake wakitumia panel za sandawij, pamoja na kuweka taa za ndani na nje, na wamejenga vyoo vyenye ukubwa wa (3*5), bamoja na kufanya ukarabati katika vyoo vingine, na kuondoa tatizo la unyevu nyevu katika kuta za haram tukufu, sambamba na kurudishia kuweka cement, huku kubba mbili tukufu zikipakwa rangi.
Idara ya mazaru tukufu pamoja na wakazi wa mji huu wametoa shukrani nyingi kwa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kufanya ujenzi na ukarabati katika mazaru hii tukufu.