Kwa ajili ya kuongeza ujuzi na kuboresha utendaji, kitengo cha habari na utamaduni kinatoa semina ya kuwajengea uwezo viongozi wa idara na ofisi zake. Semina hiyo imefanyiwa katika ukumbi wa mikutano wa kituo cha kimataifa cha masomo na utafiti Al-Ameed, ni miongoni mwa semina za kujenga uwezo zinazo fanywa na kituo cha habari na utamaduni kwa watumishi wa vitengo vyote, kila kitengo hupewa semina kutokana na sekta yake.
Ratiba ya mafunzo iliyo simamiwa na Ustadh Farasi Shimri (Mkufunzi mahiri katika sekta ya rasili mali watu na mikakati katika kitengo cha habari na utamaduni- idara ya utafiti na ubunifu), ilikua na saa nne za kukaa darasani, mada zake zilijikita katika kuangazia umihimu wa watumishi kujiendeleza kielimu ili waweze kutoa huduma bora zaidi katika kazi zao, hali kadhalika wameangalia umihimu wa kua na mpango mkakati wa kila kitengo kwa ajili ya kurahisisha utendaji wao, na kuhakikisha wanaboresha utendaji wao.
Washiriki wa semina wamesisitiza umihimu wa semina za aina hii na wamesema kua zina msaada mkubwa katika kuwajengea uwezo na kuendeleza vipaji vyao pamoja na kuboresha utendaji wa majukumu yao kwa mtu mmoja mmoja na hatiamae kufanikiwa kufikia malengo kwa ubora na ufanisi mkubwa.