Kitengo cha maadhimisho na mawakibu (vikundi) vya Husseiniyya wafanya maonyesho ya picha ya awamu ya pili katika malalo ya Imamu Ridhwa (a.s)…

Maoni katika picha
Baada ya kukamilisha hatua ya kwanza ya maonyesho ya picha katika malalo ya bibi Fatuma Maasuma (a.s) Mjini Qum, kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya cha Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) kimeanza awamu ya pili ya maonyesho hayo katika ukumbi mtukufu wa malalo ya Ghariib (mgeni) wa Tusi Imamu Ridhwaa (a.s), katika mji wa Mashhadi nchini Iran kwenye uwanja wa Ghadiir, maonyesho hayo yalihusisha picha za mnato zinazo onyesha matukio ya ziara ya Ashura na Arubaini pamoja na huduma zinazo tolewa kwa mazuwaru.

Maonyesho haya yamefanywa chini ya kauli mbiu isemayo (Mwenyezi Mungu amrehemu atakaye huisha jambo letu), yalipambwa na mbao za picha zipatazo 53, zilizo pangwa kwa umaridadi na ufanisi mkubwa, picha hizo ni za matukio mbalimbali katika ziara ya Imamu Hussein (a.s) zilizo pigwa ndani na nje ya mji mtukufu wa Karbala, katika matembezi na huduma mbalimbali ambazo hutolewa kwa mazuwaru kwenye msimu wa Ashura na Arubaini, kwa kupitia picha hizi, watu wanaona namna ambavyo hufanywa maadhimisho ya Imamu Hussein (a.s) katika mji mtukufu wa Karbala na katika Ataba takatifu.

Maonyesho yamefungua mlango wa maarifa kwa wapenzi wa Imamu Hussein (a.s) na harakati yake, watu wameuliza maswali mbalimbali, hii ni dalili nzuri ya uwelewa walio nao pia walitaka kuhakikisha mambo waliyo kua wakiyaona katika luninga (tv) zao.

Maonyesho haya yamepata mahudhurio makubwa kutoka kwa wakazi wa mji wa Qum na mazuwaru watukufu, baadhi ya watu wameomba maonyesho haya yafanyike pia katika mikoa mingine ya Iran, hususan baada ya kuongeza vipengele vingine, kama vile matembezi na muhanga wa Imamu Hussein (a.s), wakabainisha kua kila walicho kiona kinahitaji pongezi kubwa, na wakatoa shukrani nyingi kwa wahudumu wa maonyesho haya kwa kuwapa fursa ya kutambua yanayo fanyika katika ziara ya Ashura na Arubaini pamoja na huduma wanazo pewa mazuwaru watukufu katika ziara hizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: