Yametolewa maelezo kwa ufupi kuhusu masharti na mada zitakazo wasilishwa katika kongamano hilo, kama ifuatavyo:
- 1- Athari za misingi ya Ashura katika kudumisha fatwa tukufu ya kujilinda.
- 2- Baina ya mihadhara ya dini ya misimamo mikali na ya kawaida/ mihadhara ya kisasa kuhusu jihadi kama mfano (darasa mjadala).
- 3- Mazingira na athari yake kufuatia kutangazwa fatwa ya kujilinda ndani ya maeneo matakatifu/ (darasa mjadala) baina ya Karbala ya jana na ya leo.
- 4- Mtazamo wa vyombo vya habari vya kimagharibi kuhusu fatwa ya kujilinda na matokeo yake.
- 5- Athari ya fatwa katika kuzima fitna na ubaguzi na kusaidia kuunganisha umoja wa kitaifa.
- 6- Mchango wa mwanamke wa Ashura katika kulinda maeneo matakatifu.
- 7- Athari ya vyombo vya habari katika kufanikisha ushindi.
- 8- Athari ya misingi ya imani katika kujenga moyo wa jihadi/ Bariri bun Khadhiri (a.s) kama mfano.
- 9- Athari ya malezi mema katika kumjenga mtu/ Ummul-Banina (a.s) kama mfano.
- 10- Haki za binadamu baina ya uwelewa wa Ashura na Marjaaa dini ukilinganisha na uwelewa wa umoja wa mataifa (darasa mjadala).
- 11- Sifa za kiongozi na uongozi baina ya kushinda na kushindwa, kwa kulinganisha na uongozi wa Hashdi ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kama mfano (darasa mjadala kwa kuangalia mitazamo ya kimkakati).
- 12- Athari ya dua katika kuimarisha moyo wa imani kwa Mujahidi/ Dua Thughuur katika kitabu cha Sahifa Sajjaadiyyah kama mfano.
Kamati ya maandalizi imetoa orodha ya masharti yanayo hitajika katika tafiti zitakazo wasilishwa katika shindano la kongamano lijalo, kama yafuatavyo:
- 1- Utafiti usiwe umesha wahi kuandikwa au kutolewa na watu wengine kabla yako.
- 2- Utafiti uandikwe kwa kufuata kanuni za kielimu.
- 3- Zisiwe chini ya kurasa (15) na zisizidi (30), ukubwa wa maandishi uwe saizi (14) hati ya (Arabic simplified) na uwekwe kwenye (CD).
- 4- Uambatanishwe na muhtasari wake usiozidi maneno (300).
- 5- Utafiti wowote ambao hautazingazia mada tulizo taja hapo juu au hauta ambatanishwa na wasifu (CV) ya muandishi hautakubaliwa.
- 6- Tafiti zitumwe pamoja na mihtasari yake, wasifu wa muandishi, picha ndogo (paspoti saizi) za muandishi, pamoja na namba ya simu na anuani ya parua pepe, kwa kutumia barua pepe au kwa kuletwa moja kwa moja katika kitengo cha maarifa cha Atabatu Abbasiyya tukufu, au katika taasisi ya maarifa ya Nahju Balagha katika Atabatu Husseiniyya tukufu hadi mwezi mosi Rajamu (1 Rajabu 1439h).
Kwa kutuma utafiti wako au kupata maelezo zaidi wasiliana nasi kwa anuani zifuatazo:
rabee@alkafeel.net / almaaref@alkafeel.net / inahj.org@gmail.com
Au biga simu namba: (07728243600 au 07723757532 au 07815016633).