Miongoni mwa shughuli za kitamaduni za mwaka huu, chuo kikuu cha Mustanswiriyya kinafanya nadwa ya filamu kwa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya tukufu, leo Juma Tano (22 Rabiu-Thani 1439h) sawa na (10 Januari 2018m), katika ukumbi wa chuo, wameonyesha filamu ya (Sayyidat Quraish) iliyo tengenezwa na kituo cha Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya tukufu, filamu hiyo inaelezea historia ya maisha ya bibi Khadija (a.s).
Penbezoni mwa maonyesho hayo, zilitolewa mada kuhusu mambo matatu muhimu, ambayo ni; Anthropolojia ya kijamii, mada ya kihistoria na nyingine kuhusu vyombo vya habari, wawasilishaji wa mada hizo walikua ni: Dokta Jafari Najmu Nasru mwalimu wa kitengo cha Adabu katika kitengo cha Anthropolojia, Dokta Hanaan Ridhwa Kaabi mwalimu msaidizi katika kitivo cha Adabu kitengo cha historia, alizungumzia mtazamo wa kihistoria na nafasi ya kamera katika kuandika historia, na Dokta Aadil Haashim, mwalimu wa kitivo cha Adabu, amezungumzia nafasi ya filamu katika tathnia ya habari, ambapo alizungumzia madhumuni yanayo kusudiwa kueleweka katika fulamu, na akazichambua filamu katika upande wa kiufundi, ki-imani na kimaudhui, na akaelezea faida za filamu kihistoria, kiimani na kijamii.
Mkuu wa kitivo cha Adabu, Dokta Farida Jaasim alibainisha umuhimu wa nadwa hii na matokeo yake kiutamaduni kwa kusema kua: “Lengo kuu la nadwa hii, ni kujenga uwelewa kwa wanafunzi katika mambo ya kitamaduni, mitazamo ya vyombo vya habari na kielimu, na kuwaonyesha mchango unaotolewa na Ataba mbalimbali, hususan Atabatu Abbasiyya tukufu, kufanikiwa kwa taasisi yeyote katika ulimwengu wa leo kunategemea namna taasisi hiyo itakavyo shirikiana na taasisi zingine au jinsi inavyo shirikiana na jamii, na hili ndio jambo linalo fanywa na chuo chetu, vitu vinavyo onyeshwa na Atabtu Abbasiyya tukufu, vi vitu vya kipekee katika pande zote, kuanzia upande wa malengo hadi muundo wake katika sura ya nje”.
Akaongeza kusema kua: “Hakika sisi tunategemea kuendelea kujenga uhusiano na Ataba zote, kwa sababu kufaulu kwetu kunategemea ushirikiana na taasisi hizi za dini”.
Baada ya hapo ukafunguliwa mlango wa majadiliano kwa walimu na wanafunzi, mwisho kabisa wa nadwa hii, kitengo cha habari na utamaduni kikapewa zawadi, na mtunzi wa filamu hii pia Azhar Khamisi akapewa zawadi kutokana na juhudi yake kubwa aliyo fanya hadi kukamilisha filamu hii.