Kamati ya maandalizi ya kongamano la Rabiu Shahada yatoa wito kwa watafiti kushiriki katika shindano maalumu la kitafiti…

Miongoni mwa vikao
Kamati ya maandalizi ya kongamano la kimataifa na kiutamaduni Rabiu Shahada awamu ya kumi na nne, yatoa wito kwa waandishi na watafiti kushiriki katika shindano maalumu, ambalo ni miongoni mwa shughuli za kongamano linalo simamiwa na uongozi mkuu wa Ataba mbili tukufu (Abbasiyya na Husseiniyya) mwanzoni mwa mwezi ujao wa Shabani, ambalo ni sehemu ya kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa wajukuu wa Mtume Muhammad (a.s), litakalo fanywa chini ya kauli mbiu isemayo (Tumepigana kutokana na Hussein (a.s) na tumeshinda kutokana na fatwa).

Kamati ya maandalizi imeweka orodha ya masharti na kanuni zinazo takiwa kufatwa na watafiti watakao shiriki katika shindano la kongamano hilo kama ifuatavyo:

  • 1- Utafiti usiwe umesha wahi kuandikwa au kutolewa na watu wengine kabla yako.
  • 2- Utafiti uandikwe kwa kufuata kanuni za kielimu.
  • 3- Zisiwe chini ya kurasa (15) na zisizidi (30), ukubwa wa maandishi uwe saizi (14) hati ya (Arabic simplified) na uwekwe kwenye (CD).
  • 4- Uambatanishwe na muhtasari wake usiozidi maneno (300).
  • 5- Utafiti wowote ambao hautazingazia masharti tuliyo taja hapo juu au hauta ambatanishwa na wasifu (CV) ya muandishi hautakubaliwa.
  • 6- Tafiti zitumwe pamoja na mihtasari yake, wasifu wa muandishi, picha ndogo (paspoti saizi) za muandishi, pamoja na namba ya simu na anuani ya parua pepe, kwa kutumia barua pepe au kwa kuletwa moja kwa moja katika kitengo cha maarifa cha Atabatu Abbasiyya tukufu, au katika taasisi ya maarifa ya Nahju Balagha katika Atabatu Husseiniyya tukufu hadi mwezi mosi Rajamu (1 Rajabu 1439h).

Ifahamike kua zimeandaliwa zawadi kwa tafiti bora tatu za kwanza kama ifuatavyo:

Mshindi wa kwanza: Milioni moja na nusu (1,500,000) dinari za Iraq.

Mshindi wa pili: Milioni moja (1,000,000) dinari za Iraq.

Mshindi wa tatu: Laki saba na elfu hamsini (750,000) dinari za Iraq.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa anuani zifuatazo:

rabee@alkafeel.net / almaaref@alkafeel.net / inahj.org@gmail.com

Au biga simu namba: (07728243600 au 07723757532 au 07815016633).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: