Maahadi ya Qur’an tukufu imetoa jarida nyingi za Furqaan zinazo chapishwa na kituo cha habari za Qur’an kilicho chini yake…

Maoni katika picha
Kituo cha habari za Qur’an chini ya Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya kimetoa jarida za Furqaan kati ya (10 na 11), zinazo elezea harakati zinazo fanywa na Maahadi, pamoja na aina za visomo vya Qur’an na tafiti kuhusu Qur’an zinazo lenga kunufaisha watu wa tabaka tofauti na kutatua changamoto za kijamii.

Shekh Jawaad Nasrawi mkuu wa Maahadi ya Qur’an amesema kua: “Maahadi ya Qur’an tukufu ni miongoni mwa taasisi za Qur’an zilizo chini ya Atabatu Abbasiyya na zinazo pewa umuhimu mkubwa na kiongozi mkuu wa kisheria Sayyid Ahmadi Swafi, pamoja na uongozi mkuu, wamefanya semina za Qur’an kua miongoni mwa vipao mbele vikuu vya shughuli zao, na semina hizo hulenga watu wa rika zote, kwa ajili ya kueneza uwelewa wa Qur’an kwa jamii nzima, hivyo ikaundwa kamati ya habari iliyo fanya kazi mchana na usiku kuhakikisha inazitoa habari katika muonekano mzuri wa jarida la Furqaan.

Shekh Nasrawi akaongeza kusema kua “Hakika kila kilicho andikwa katika jarida hizi, ni mada za kitafiti zinafaa kua masomo ya bachela, masta au hata dokta (phd) lakini zimeandikwa kwa muhtasari ili ziendane na jarida hizi”.

Fahamu kua kituo cha habari za Qur’an chini ya Maahadi ya Qur’an, kina kurasa nyingi za kielektonik zinazo rusha habari za Maahadi na harakati zake kwa kupitia picha na video, jarida la Furqaan ni ukurasa mwingine mzuri utakao fikisha elimu kwa wasomaji kwa njia hii, jarida hizi zimejaa maudhui kuhusu Qur’an zilizo andikwa kwa mpangilio mzuri, pia zina makala za Qur’an kuhusu elimu ya nafsi, jamii na mengineyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: