Kwa ajili ya kuenzi damu zao tukufu, zilizo mwagika katika ardhi ya Iraq, kwa ajili ya kuhakikisha watu wanaendelea kuishi kwa utukufu baada yao, na kufuatia agizo lililo tolewa na Marjaa dini mkuu la kutaka kuenzi kumbukumbu zao, Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha habari na utamaduni, inatoa wito kwa familia za mashahidi wa Hashdi Sha’abi, waleta picha moja ya Shahidi pamoja na kitambulisho chake na maelezo yafuatayo:
1/ Majina manne na jina la sifa (laqabu).
2/ Tarehe ya kuzaliwa.
3/ Mahali alipokua anaishi.
4/ Hali yake ya kijamii na idadi ya watoto.
5/ Mahali na tarehe aliyo pata shahada.
6/ Kiwango chake cha elimu.
7/ Jina la kikosi alicho kua anapigana.
Kwa ajili ya kuingiza taarifa hizo katika kitabu (mausua) ya (Fatwa tukufu ya kujilinda) ambacho kinatarajiwa kuchapishwa miezi michache ijayo, kitakua na juzuu maalumu litakalo andika mashahidi wa Hashdi Sha’abi.
Taarifa hizo zitumwe kwa anuani ya barua pepe ifuatayo: sadda@alkafeel.net au kwa simu namba: 07808318441 kwa kutumia (Watsapp, Viber na Telegram) au kwa kupitia ukurasa wa Facebook (wa mtandao wa Alkafeel wa kimataifa).
Mwisho wa kupokea taarifa hizo ni tarehe: 28/02/2018m.