Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kujenga mahusiano mema na vyuo vikuu…

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya imeweka kipawambele sana cha kujenga mahusiano na wadau wa nje, hususan wanafunzi wa vyuo vikuu, kutoka na umuhimu wao katika jamii ya Iraq, hivyo wamefanya mambo kadhaa yanayo endana na tabaka la wanafunzi hao, kwa ajili ya kuchangia kukuza uwezo wao kielimu, kifikra na kimaadili, chini ya misingi ya kislamu na kuwafanya waweze kupambana katika vita vya kifikra na kiutamaduni.

Idara ya mahusiano na vyuo vikuu kupitia mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel, imebeba jukumu hilo na imesha fanya shughuli nyingi, baadhi hufanywa katika vyuo vikuu na zingine hufanywa hapa Atabatu Abbasiyya, kukaribisha wanafunzi wa vyuo na Maahadi za Iraq, ni moja ya shughuli hizo, ni shughuli ya kimatembezi yenye mambo mengi, hufanywa kwa kuwasiliana na marais wa vyuo na kukubaliana nao kuhusu muda na ratiba kamili, pamoja na kuhakikisha wanafunzi wengi zaidi wanapata nafasi hiyo.

Kama tulivyo sema matembezi haya hujumuisha vitu vingi na hupangiliwa kwa kushirikiana na vitengo vingine vya Ataba, katika matembezi ya safari hii yamejumuisha mambo yafuatayo:

  • - Kuzuru malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa pamoja.
  • - Kutembelea baadhi ya miradi ya Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) pamoja na kutembelea baadhi ya vitengo vya Ataba hizo na kupata maelezo kutoka kwa watumishi.
  • - Kusikiliza mihadhara mbalimbali, ya Fiqhi, Akhlaq na Aqida inayo endana na umri wao, na kujibu maswali au kutoa maelezo zaidi katika mambo yanayo husu maisha yao ya chuo, familia na katika jamii.
  • - Kusikiliza mihadhara kuhusu maendeleo ya binadamu, inayo lenga kujenga uwelewa wa jumla kwa wanafunzi kuhusu maendeleo.

Kumbuka kua mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel, ni mradi wa kielimu na kimalezi, unalenga kuongeza uwezo wa vijana waliopo vyuoni na kwenye Maahadi hapa Iraq katika sekta mbalimbali, na kuwafanya kua vijana wenye kujitambua na wapenzi wa Ahlulbait (a.s), na kumuwezesha kua na utamaduni pamoja na uwezo wa kuijenga nchi yake, pia kumsaidia kufahamu hatari zinazo tishia taifa letu na maslahi ya uislamu siku zijazo, idara ya mahusiano katika kitengo kikuu cha mahusiano ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, inafanya program (shughuli) nyingi zinazo lenga kumjenga mwanafunzi na kumuwezesha kuwa mtu bora anaye ishi kwa kufuata mwenendo na mafundisho ya Mtume (w.a.w.w) pamoja na Ahlulbait (a.s) sambamba ya kujengo moyo wa uzalendo wa taifa lao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: