Kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimetumia zaidi ya dinari bilioni maoja kwa ajili ya kuwasaidia wapiganaji wa kujitolea na mashahidi wao pamoja na majeruhi katika mwaka wa 2017m…

Maoni katika picha
Kitengo cha dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kua; katika kipindi cha mwaka wa (2017 miladiyya) kimetumia kiasi ya riali za Iraq (1,410,744,000) bilioni moja na milioni mia nne na kumi, laki saba na arubaini na nne elfu dinari, zinajumuisha misaada ya vifaa na kimkakati.

Pesa yote hiyo ilikusanywa kutoka katika masanduku ya michango ya Alkafeel, yaliyo simamiwa na kamati maalumu chini ya kitengo cha dini, wao ndio walio yaandaa, wakayasambaza na ndio walio kua wanayafungua na kuhesabu pesa iliyo patikana, kwa kufuata utaratibu ulio wekwa tangu kutolewa kwa fatwa tukufu ya kujilinda, iliyo pelekea kukombolewa kwa miji yote ya Iraq mwaka wa (2017m) kutoka mikononi mwa magaidi wa Daesh, kwa mujibu wa maelezo ya kitengo cha dini, misaada iliyo tolewa ilikua kama ifuatavyo:

  • 1- Kusaidia jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi kwa kuwapa vifaa na kuwajenga moyo wa kupambana katika uwanja wa vita kimetumika kiasi cha (1,046,744,000) bilioni moja na milioni arubaini na sita, laki saba na arubaini na nne elfu dinari za Iraq, ilihusisha kununua nguo za jeshi, nguo za kawaida, ngoa za mvua na vyakula mbalimbali, maji, barafu pamoja na dawa muhimu za aina mbalimbali na simu mafuta uzuri na kufungua sehemu za kutengeneza mikate na sehemu za kutengeneza barafu, pamoja na vitu vingine vingi nafasi haitoshi kutaja kila kitu.
  • 2- Kutoa zawadi kwa familia za mashahidi, ambapo jumla ya familia (454) zimenufaika na mradi huu, kiasi cha jumla ya pesa iliyo tumika ni (313,000,000) milioni mia tatu kumi na tatu, walipewa zawadi hizo kwa kuwatembelea katika miji yao au kwa kuandaa tamasha ndani au nje ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
  • 3- Kutoa zawadi kwa majeruhi wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi wakiwa katika miji yao au maeneo wanako patia matibabu, majeruhi (102) wamenufaika na mradi huu, jumla ya pesa iliyo tumika ni (51,000,0000) milioni hamsini na moja, misaada yote ilitolewa kwa kufuata utaratibu maalumu ulio andaliwa na viongozi wa kitengo husika.

Kumbuka kua lengo la misaada hii lilikua ni kuwashajihisha wale walio itikia wito wa Marjaa dini mkuu, wa kuwataka wajitolee kuilinda Iraq na maeneo matakatifu, na kufanyia kazi maelekezo ya Marjaa dini mkuu yaliyo sisitiza kuwasaidia wapiganaji wa serikali na Hashdi Sha’abi katika uwanja wa vita dhidi ya maadui wa Mwenyezi Mungu na Ubinadamu, vita ambayo ilihitaji juhudi za ziada ili kuwashinda maadui hao, ukizingatia kua Hashdi Sha’abi walikua na upungufu mkubwa wa mali na vifaa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: