Atabatu Abbasiyya yashiriki katika maonyesho ya (Viwanda vya Iraq) yanayo fanyika katika mji mkuu Bagdad…

Maoni katika picha
Asubuhi ya leo Juma Tatu ya (27 Rabiu-Thani 1439h) sawa na (15 Januari 2018m) yameanza maonyesho ya (Viwanda vya Iraq) yanayo simamiwa na wizara ya viwanda na madini ya Iraq, katika mji mkuu Bagdad awamu ya tatu, itakayo dumu siku nne, Atabatu Abbasiyya tukufu imepata fursa ya kushiriki katika maonyesho hayo kupitia (shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud na Darul-Kafeel ya uchapishaji na usambazaji, pamoja na kiwanda cha kutengeneza nguzo na kile cha kutengeneza kokoto) na wamepata mwitikio mkubwa kutoka kwa watu walio tembelea maonyesho haya.

Waziri wa viwanda na madini Muhandisi Muhammad Shiyaa Sudani, amewasifu wawakilishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika maonyesho haya, alipo tembelea vibanda (korido) zao baada ya ufunguzi wa maonyesho, akasema kua: “Hakika kutengenezwa kwa bidhaa tofauti ni jibu kwa tatizo la msingi katika sekta ya uchumi, na matawi ya Atabatu Abbasiyya tukufu ni fahari kubwa kwetu, ni kimbilio pekee la bidhaa za kilimo hapa nchini hususan katika sekta ya mbolea”.

Muhandisi Aadil Maliki mkuu wa shirika kuu la uchumi la Alkafeel, amesema kua: “Kutokana na umuhimu wa maonyesho haya, kwa mara ya kwanza Atabatu Abbasiyya imeshiriki katika maonyesho ya viwanda, kupitia vituo vyake vya uzalishaji na uchumi, na chini ya kauli mbiu yake ya, saidia uzalishaji wa viwanda vya Iraq”.

Akaonyeza kusema kua: “Matawi ya Atabatu Abbasiyya yamepambwa na bidhaa mbalimbali, kila tawi limeweka bidhaa wanazo tengeneza, Atabatu Abbasiyya tukufu imeshiriki katika maonyesho haya kwa ajili ya kuonyesha ubunifu na maendeleo ya vitengo vyake katika sekta ya viwanda, kilimo na uzalishaji wa chakula, pamoja na kuangalia bidhaa zinazo tengenezwa na viwanda vingine, pia hii ni fursa kubwa ya kuwasiliana na mashirika ya kitaifa yanayo shiriki katika maonyesho”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imesha shiriki mara nyingi katika maonyesho ya aina hii, ikiwa ni pamoja na maonyesho ya kimataifa ya Bagdad, pamoja na maonyesho na makongamano yaliyo fanywa ndani na nje ya Iraq, yanayo lenga kuonyesha maendeleo yaliyo patikana katika vitengo vyake kwenye sekta zote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: