Ugeni kutoka ofisi ya usimamizi wa mali watembelea Atabatu Abbasiyya tukufu, na wakutana na kiongozi mkuu wa kisheria pamoja na katibu mkuu na waonyesha kufurahishwa na miradi ya Ataba…

Maoni katika picha
Kwa ajili ya kujenga ushirikiano, ujumbe kutoka ofisi ya usimamizi wa mali za muungano, umetembelea Atabatu Abbasiyya tukufu na kukutana na kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi pamoja na katibu mkuu Mhandisi Muhammad Ashiqar, na wameangalia miradi ya Ataba, na huduma zinazo tolewa na Ataba hapa nchini, katika ziara hii wamezungumzia swala la kuimarisha uhusiano na wizara.

Dokta Swalahu Nuri Khalf rais wa ofisi ya usimamizi wa mali za muungano, ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hakika huduma zinazo tolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu zina mchango mkubwa sana katika uchumi wa taifa, kuna kitu kinaitwa himaya ya kijamii, imeboresha maisha ya zaidi ya familia (8000), bidhaa wanazo zalisha zina ubora wa hali ya juu na zinakidhi haja kwa kiasi kikubwa, zinachangia asilimia kubwa ya uwezo wa kujitegemea wenyewe, tunaweza kutoa ushauri kwa baraza la mawaziri na wizara mbalimbali wanunue bidhaa hizi”.

Akaongeza kusema kua: “Hakika Atabatu Abbasiyya tukufu, kutokana na huduma inazo toa kwa jamii, kuanzia huduma za afya, kilimo na vifaa vya viwandani, tayali imepiga hatua kubwa sana katika kulitumikia taifa kwa ujumla, kwa maana hiyo; Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na Ataba zingine, sio taasisi za kutoa maelekezo ya dini peke yake, bali zinatoa mafundisho ya dini, elimu mbalimbali na mafundisho ya kiutamaduni, zina mchango mkubwa katika kujenga jamii na kuiendeleza kiuchumi”.

Akaendelea kusema kua: “ukilindanisha na taasisi za serikali ya Iraq, utaona zinarudi nyuma kila siku, lakini Atabatu Abbasiyya tukufu inaenda na wakati, imepiga hatua kubwa katika sekta ya maendeleo, sehemu kubwa ya bidhaa za ndani zinazalishwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa sasa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: