Maahadi ya Qur’an tukufu yampongeza mmoja wa wasomi wake aliye jiandaa kushiriki katika shindano la dunia…

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya imetoa pongezi kwa bwana Hassan Alaa Dhabhawi, ambaye amejiandaa kushiriki shindano la Qur’an la dunia baada ya kuibuka mshindi katika mashindano ya Iraq, kupitia hafla kubwa ya Qur’an iliyo fanywa katika wilaya ya Hindiyya, na kuhudhuriwa na watu wengi miongoni mwa wakazi wa mji huo na viongozi wa kijamii pamoja na wadau mbalimbali wa Qur’an.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu iliyo somwa na Yusufu Fatalawi, baada ya ufunguzi huo; mkuu wa kitivo cha elimu ya kiislamu katika chuo kikuu cha Baabil Dokta Ali Abdulfataah Hasanawi alizungumza kuhusu utukufu wa Qur’an, na umuhimu wa kushikamana nayo pamoja na kuifanya kua ndio katiba na muongozo wa kila anayetaka mafanikio, akafafanua kua; Maahadi ya Qur’an tukufu tawi la wilaya ya Hindiyya limekua na nafasi kubwa katika kufundisha Qur’an kila sehemu ya wilaya hii.

Kisha ukafuata ujumbe wa Sayyid Haamid Mar’abi ambaye ni kiongozi wa tawi hili, aliwakaribisha wahudhuriaji na akaelezea shughuli zinazo fanywa na tawi hili ambazo miongoni mwa matunda yake ni kupatikana kwa msomi huyu atakaye shiriki mashindano ya dunia.

Baada yake ilifuata Qur’an tukufu iliyo somwa na msomi wa kimataifa Sayyid Hassanain Halo, iliyo burudisha masikio ya wahudhuriaji, hafla ikapambwa kwa kaswida murua za kidini zilizo elezea utukufu wa Qur’an.

Mwisho kabisa akasoma Qur’an mpongezwaji Sayyid Hassan Dhabhawi.

Idara ya Maahadi ya Qur’an tukufu pamoja na wahuduriaji wote wanamtakia mafanikio katika shindano la dunia msomi wetu na tunategemea ainue jina la Iraq katika shindano hilo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: