Shirika la usalama la Alkafeel lafungua milango yake kwa mabalozi wa elimu na lasisitiza kua milango yake itaendelea kua wazi kwa wanafunzi wa tabaka zote…

Maoni katika picha
Shirika la usalama la Alkafeel limeweka utaratibu wa kupokea wanafinzi wa ngazi zote, kuanzia wanafunzi wa shule za msingi hadi wa vyuo, kila wakati wanapokea mabalozi wa elimu (wanafunzi) kutoka shule mbalimbali wanaokuja kutembelea shirika hili, na limetenga muda mwingi kwa ajili ya kufanikisha zoezi hilo la matembezi ya wanafunzi, yanayo changia kukuza uwezo wao wa akili, hivi karibuni wamepokea wanafunzi kutoka shule ya Mauhubiin iliyopo katika mkoa mtukufu wa Najafu.

Mkuu wa kamati ya utendaji ya shirika hili amewahimiza wanafunzi kuongeza bidii katika masomo na kuhakikisha wanafaulu, jambo ambalo linategemewa na wazazi wao, ili waweze kulitumikia taifa kwani wao ndio viongozi wa kesho.

Ziara hii ilihusisha kutembelea sehemu mbalimbali za shirika, na walipewa nafasi ya kuuliza maswali kwa watumishi.

Uongozi wa shirika umezikaribisha taasisi zote za elimu kuja kulitembelea na kuangalia untendaji wake, ukizingatia kua ni shirika la kiiraq linye nafasi kubwa katika sekta ya mawasiliano, na milango yake iko wazi kwa wanafunzi wa tabaka zote.

Kumbuka kua mkuu wa kamati ya utendaji Muhandisi Aarif Bahashi amesha sema katika tamko lake kua: “Hakika shirika linafanya kila linalo wezekana kuhakikisha linatoa huduma bora za mawasiliano kwa watu walio onyesha uaminifu kwao, linafanya kazi kwa kufuata maelekezo ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na kiongozi wake mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, kwa lengo la kuhakikisha linaondoa mzigo mkubwa kwa raia wa kulipa gharama zilizo wekwa na mashirika likiwemo shirika hili pia”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: