Kitengo cha utunzaji wa haram tukufu chafanya usafi katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)…

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo cha utunzaji wa haram tukufu chini ya uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, na kwa kushirikiana na vitengo vingine, wameanza kusafisha haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuhakikisha wanailinda na uharibifu wowote.

Kukosi kazi cha usafi kimechagua kufanya shughuli zao usiku mwingi, kwa ajili ya kuepuka kuwasumbua watu wanaokuja kufanya ziara, pia wakati huo ni rahisi kufanya kazi zao kwa uhuru, baaba ya kumaliza kuosha kwa maji, huyakausha kisha hutandika mazulia na kupulizia manukato ndani ya haram tukufu.

Kumbuka kua kitengo cha utunzaji wa haram hufanya usafi kila baada ya muda fulani, kutokana na utukufu wa eneo hili, wanahakikisha lipo safi muda wote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: