Mwitikio chanya wapatikana katika tawi la shirika la teknelojia ya kilimo cha kisasa Aljuud, lililo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu linalo shiriki katika maonyesho ya viwanda yaliyo pewa jina la (Viwanda vya Iraq), yalio andaliwa na shirika la kazi za maonyesho ya kimataifa chini ya wizara ya viwanda na madini katika uwanja wa maonyesho ya kimataifa mjini Bagdad chini ya kauli mbiu isemayo: (Viwanda vyetu ndio utaifa wetu na amani yetu na uhuru wetu wa daima), mwitikio huo unatoka kwa watu wa aina zote, wa ndani na nje ya nchi, kupitia ugeni unao tembelea tawi hii na kuangalia bidhaa zake za kilimo na za viwandani.
Tawi hili –pamoja na kwamba linashiriki kwa mara ya kwanza katika maonyesho haya- limekua kituo muhimu kwa watu wanaokuja kutembelea maonyesho haya, kila mtu anaye tembelea maonyesho haya anavutiwa na tawi hili pamoja na matawi mengine ya Atabatu Abbasiyya tukufu, huja kubadilishana mawazo na kujadili njia za kushirikiana baina yao na shirika la Juud pamoja na kutoa pongezi kubwa kwa viongozi wote, kutokana na maendeleo yanayo shuhudiwa katika ataba ya kiviwanda na sekta zingine ambayo ni nguzo muhimu kwa uchumi wa taifa.
Waziri wa viwanda na madini Muhandisi Muhammad Shiyaa Sudani, amesifu bidhaa zinazo onyeshwa pamoja na juhudi zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya ya kurudisha uhai katika sekta ya viwanda vya Iraq, sambamba na ubora wa bidhaa wanazo tengeneza, akabainisha kua uwepo wa bidhaa za aina tofauti katika matawi ya Atabatu Abbasiyya tukufu ni fahari kwa kubwa kwa uzalishaji wa viwanda vya ndani.
Ugeni kutoka katika ubalozi wa Japani wa hapa Iraq, -walipo tembelea tawi hili na kuangalia bidhaa zake na baada ya kupata maelezo kuhusu bidhaa hizo- wameonyesha utayari wao wa kushirikiana na kubadilishana uzowefu pamoja na kuangalia njia za kuboresha zaidi uzalishaji jambo ambalo litachangia sana kukuza uchumi wa Iraq katika kipindi hiki muhimu.
Kwa ufupi watu wote walio tembelea na kuangalia bidhaa zinazo zalishwa na viwanda vyetu, wameridhishwa na bidhaa na wameonyesha moyo wa kununua bidhaa hizo kwani zinakidhi mahitaji yao, tunatarajia kuongezeka kwa kiwango cha mauzo katika bidhaa zetu.