Kufungua mlango wa kushiriki katika program ya Rabiu Maarifa ya Skaut awamu ya pili…

Maoni katika picha
Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel chini ya idara ya watoto na makuzi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kuanza usajili kwa wanaotaka kushiriki katika program ya (Rabiu Maarifa ya Skaut awamu ya pili), itakayo anza katika kipindi cha likizo, program hiyo itakua na mambo mbalimbali kama yalivyo pangwa na kamati husika, yanayo lenga kuinua kiwango cha kujitambua kifikra na kiutamaduni, pamoja na kubaini vipaji na kuangalia njia ya kuviendeleza.

Program hii inalenga rika za aina tatu ambazo ni:

Kwanza: Kuanzia umri wa miaka 10 hadi 12 (Darasa la tano na la sita la shule za msingi).

Pili: Kuanzia umri wa miaka 13 hadi 15 (Darasa la kwanza, la pili na la tatu la shule za sekondari (A.levo)).

Tatu: Kuanzia umri wa miaka 16 hadi 18 (Darasa la nne hadi la sita la sekondari (O. levo)).

Program ya Skaut Rabiu Maarifa itakua na mambo mengi, na itachukua siku kumi, miongoni mwa mambo yatakayo fanyika ni:

  • - Kufunga hema za Skaut.
  • - Kutakua na michezo mbalimbali.
  • - Kutakua na kazi ndogondoga kwa ajili ya kuongeza uwezo wa akili na mwili.
  • - Safari za kimasomo na kimapumziko.
  • - Kazi za kielimu na kitamaduni.

Mkazi wa mkoa wa Karbala na wilaya zake anaye penda kushiriki program hii, atembelee jengo la Imamu Hassan Askariyyu (a.s) lililokua likijulikana kama (Funduq Dalla), lililopo katika mlango wa Bagdad, na kwa maelezo zaidi piga simu ifuatayo: (07602326690) fahamu kua nafasi ni chache na usajili unaendelea hadi mwanzoni mwa mwezi ujao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: