Shule za Ameed zilizo chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, zimekidhi vigezo vyote ndani ya muda ulio pangwa, na kua mfano bora kimalezi na kielimu kwa kiwango cha taifa, zimestahiki kupata heshima hiyo kutokana na juhudi za watendaji wake pamoja na umakini wa viongozi na wasaidizi wao, wote kwa pamoja wanafanya kazi kwa bidii kufikia lengo moja tu, nalo ni kuboresha shule zao na kuzifanya kua za kupigiwa mfano.
Wameanza kusajili wanafunzi katika shule zao kumi na nne, ambazo ni: (Shule ya msingi Al-Ameed ya wasichana, Shule wa msingi Al-Ameed ya wavulana, Shule ya msingi Al-Qamar ya wasichana, Shule ya msingi Saaqi ya wavulana, Shule ya msingi Sayyidul-Maa ya wavulana, Shule ya msingi Nurul-Ameed ya wavulana, Shule ya msingi Nurul-Abbasi (a.s) ya wavulana, Shule ya msingi Nurul-Abbasi (a.s) ya wasichana, Shule ya sekondari ya Nurul-Abbasi (a.s) ya wasichana, Shule ya Abu Twalib (a.s) ya masomo ya msingi kwa wanaume, Shule ya sekondari ya Sayyidul-Maa ya wavulana, na sekondari ya Ameed ya wasichana) pamoja na shule zake tatu za awali: (Shule ya awali ya Saaqi, Ameed na Nurul-Abbasi (a.s)) shule hizi zinamazingira bora zaidi ya kimalezi na kielimu.
Dokta Mushtaaq Ali, msaidizi wa kitengo cha malezi na elimu ya juu ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hakika maonbi ya wanafunzi wanaotaka kujiunga na shule zetu yamezidi uwezo wa shule tulio nao kwa sasa, jambo hili lilitarajiwa kutokana na mazingira bora ya kimalezi na kielimu yaliyopo katika shule zetu, tuna walimu bora na tunafundisha vizuri, kwa kutumia vifaa vya kisasa vinavyo tumika katika nchi zilizo endelea, pamoja na kulinda misingi yetu ya kiislamu na utamaduni wetu, na tuna selebasi nzuri, kila shule inamshauri mkuu wa mambo ya kimalezi aliye bobea katika sekta hiyo, pia idara zetu za shule zina ushirikiano mkubwa na hukaa pamoja na kujadili namna ya kupambana na changamoto zinazo weza kujitokeza, sambamba na kuainisha mambo yanayo saidia kujenga mustakbali mwema wa watoto).
Akaongeza kusema kua: “Hakika tunafanya kazi kwa kufuata utaratibu maalumu, kwa ajili ya kuhakikisha tunatoa huduma bora za kimalezi na kielimu kwa idadi kubwa zaidi kadri itakavyo wezekana, kwa ajili ya kutumikia taifa letu na kutekeleza maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya hivi sasa inajenga vituo viwili vikubwa vya elimu, kimoja kipo katika barabara ya mji wa Huru (a.s), pana eneo kubwa, patakua na shule za kawaida tano na shule za awali mbili, na kituo cha utamaduni na kumbi nne za michezo, jengo lingine, linajengwa karibu na malalo ya Huru (a.s), litakua na shule tatu za kawaida, na moja ya awali pamoja na ukumbi wa michezo.