Atabatu Abbasiyya yakarabati sistim ya umeme na sauti pamoja na kusafisha malalo ya bibi Zainabu (a.s)…

Maoni katika picha
Kutokana na maelekezo ya Mheshimiwa Sayyid Ahmad Swafi kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na kutokana na msaada wa uongozi wa Ataba tukufu, ujumbe wa Atabatu Abbasiyya ulio kwenda katika malalo ya bibi Zainabu (a.s) umekamilisha hatua ya tatu ya ukarabati wa malalo tukufu kwa kuisafisha na kuipamba.

Ujumbe ulio kwenda katika haram ya Aqilah Twahirah (a.s) na kuchukua jukumu la kukamilisha kazi zote za kukarabati, kusafisha na kupamba kuta za haram tukufu pamoja na milango ya fedha inayo ingia katika haram, na kusafisha maraya (marumaru za vioo) na kukarabati mapambo, pamoja na kutengeneza upya sistim ya sauti, kukarabati saa na kuweka plastiki sehemu za milangoni kwa ajili ya kuzilinda zisiharibike na joto, na kukarabati vyumba vya mitambo ya umeme kwa kuvifunika kwa mbao, ujumbe huo umefanikiwa kumaliza kazi ndani ya muda mfupi, wametumia siku tano tu, wamefanya kazi mfululizo usiku na mchana.

Ujumbe huo pia ulifanya kazi za ziada, hayo yalisimuliwa na bwana Hassan Hilali rais wa kitengo cha utunzaji wa haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya, aliye kua kiongozi wa ujumbe huo, alisema kua: “Watalamu wetu walitelemsha mapambo yote yaliyo kuwepo juu ya kaburi na kuyasafisha pamoja na kutengeneza taa zilizo kua zimeharibika ili kuyarudisha katika muonekano mzuri, baada ya hapo wakaanza kusafisha kaburi na kulifanyia ukarabati kamili kazi iliyo dumu siku mbili, pamoja na kukarabati mauwa yaliyo juu ya kaburi, na kuyafanya kua na muonekano mzuri, kazi hii ilihusisha mapambo yaliyopo katika korido za haramu pia, pamoja na kusafisha maraya za ndani”.

Akaongeza kusema kua: “Kazi kubwa ilikua ni kutoa umeme katika kituo kikuu hadi katika malalo ya bibi Zainabu (a.s) baada ya kua walikua wanategemea umeme unaotoka katika kituo cha Daizul peke yake, Alhamdu lilaahi, tumefanikiwa kuunganisha umeme kwa umbali wa mita (70) pamoja na kufunga fesi kubwa pamoja na kukarabati vyumba vyinavyo tunza umeme kwa kushirikiana na sekta maalumu za Sirya”.

Rais wa ujumbe huo akabainisha kua: “Tumefunga spika katika kituo cha matangazo na kufungua kituo cha walio potelewa (mafqudiin) na kuweka mitambo ya spika ya kisasa zaidi, pamoja na kuweka taa za mapambo kwa ajili ya kujiandaa na kumbukumbu ya kuzaliwa kwa bibi Zahraa na bibi Zainabu (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: