Hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya kwa mafanikio upasuaji zaidi ya 170 wa maradhi ya moyo na kubadilisha mishipa tangu kufunguliwa kwake, upasuaji huo ni miongoni mwa upasuaji mgumu zaidi, hapo awali ulikua ukifanyika nje ya Iraq na kuwagharimu wairaq pesa nyingi pamoja na kwamba matibabu hayakua na uhakika.
Na kwa upande mwingine madaktari wetu walifanikiwa kufanya zaidi ya upasuaji wa macho 1000 na wote ulifanikiwa, upasuaji wote uliofanywa, madaktari wa kiiraq walikua na mchango mkubwa wa kufanikisha, na baadhi yake ulifanywa na madaktari wa kiiraq peke yao bila kushirikiana na madaktari wa kigeni.
Fahamu kua, kuna aina mbalimbali za matibabu ya kituruki –Ambayo ni sehemu ya matibabu yaliyo fanywa na hospitali ya Alkafeel- na walifanya hafla ya kusherehekea mafanikio hayo, mkuu wa jopo la madaktari Nuri Bolo amebainisha kua; wamefanya hafla ya kusherehekea mafanikio ya upasuaji wa moyo yanayo simamiwa na daktari wa kituruki Bashiri Akbanari, kwa kufanya upasuaji wa mafanikio kwa wagonjwa mia moja wa moyo, na wengine zaidi ya sabini walio badilishwa mishipa, na hakuna hata upasuaji mmoja ulio feli, akabainisha kua: madaktari wa kiiraq pamoja na wauguzi walikua msingi mkubwa katika kufanikisha matibabu yaliyo fanyika na sisi tunajivunia wao.
Kumbuka kua hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu wamesha fanya mamia ya upasuaji wa magonjwa mbalimbali na asilimia kubwa walifanikiwa, hii inatokana na sababu kuu mbili: Utalamu wa madaktari wa kiiraq na wa kigeni waliopo katika hospitali hii, na uwepo wa vifaa tiba bora na vya kisasa, kwa kupatikana vitu hivyo viwili ukiongeza na baraka za mwenye jina tukufu la hospitali ya Alkafeel, ambaye ni Abulfadhil Abbasi (a.s).
Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zinazo tolewa na hospitali, unaweza kuangalia toghuti ya hospitali ifuatayo: www.kh.iq au piga simu namba (07602344444) au (07602329999).