Kutokana na utalamu wa wairaq na watumishi wa Abbasi, mlango wa Hamdi unanyoosha mikono yake kukaribisha wageni wa malamo ya Sayyid Muhammad (a.s)…

Maoni katika picha
Baada ya kumaliza kutengeneza mlango mpya wa malalo ya Sayyid Muhammad bun Imamu Ali Haadi (a.s) (Mlango wa Hamdi) ulio tengenezwa katika kiwanda cha Atabatu Abbasiyya tukufu cha kutengeneza milango na madirisha ya makaburi na mazaru tukufu, ili uchukue nafasi ya mlango ulioharibika katika shambulizi lililofanywa na magaidi mwezi wa saba mwaka 2016m, na umetolewa kama zawadi kutoka kwa watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), mafundi na wahandisi wa Ataba tukufu wamefanya kazi ya kuweka mlango huo, usimame kwa utukufu wa mwenye malalo hii takatifu na unyooshe mikono kuwapokea watu wanaokuja kufanya ziara.

Hafla ya mnasaba huu imefanywa karibu na mlango wa malalo katika mji wa Balad, na kuhudhuriwa na wakazi wengi wa mji huu pamoja na watumishi wa malalo hiyo tukufu na wawakilishi wa Maraajii dini katika wilaya hii, baada ya Qur’an ya ufunguzi, ulifuata ujumbe wa uongozi wa mazaru hiyo, ulio wasilishwa na katibu mkuu bwana Abbasi Abdu-Ali, ambae alianza kwa kutoa shukrani kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kutengeneza mlango huu (mlango wa Hamdi), ambapo wamefanya kazi hiyo kwa ajili ya kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu mtukufu na kutokana na mapenzi yao kwa watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w), hakika mlango huu una nafasi kubwa kwa watu wanokuja kufanya ziara katika eneo hili tukufu, na akatoa shukrani kwa wakazi wa Balad ambao wamefurahi sana kurudi kwa mlango ukiwa katika hali bora zaidi, na kuletwa kwa mlango huu ni jibu kwa magaidi walio kusudia kuvunja malalo hii tukufu, hakika mlango huu uliontengenezwa na Atabatu Abbasiyya tukufu ni michache sana milango kama hii, huu ni mlango wa kwanza kutengenezwa wenye sifa kama hizi, lakini hili sio jambo geni kwa Ataba tukufu, kwani wana uzowefu mkubwa wa kutengeneza milango ya Ataba na Mazaru tukufu, na wamesha toa michango mingi katika malalo hii tukufu na sasa wametoa mlango wa Hamdi, tunawashukuru sana Atabatu Abbasiyya tukufu na watumishi wake, watapata thawabu na malipo makubwa kutokana na utukufu wa mwenye malalo hii na utukufu wa Ammi yake Imamu wa zama (a.f).

Mwakilishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na rais wa msafara, aliye simamia ubebaji wa mlango huo kutoka Karbala hadi Balad, Ustadh Ali Swafaar aliongea kua: “Tuna furaha kubwa sana kufanikiwa kutumikia malalo ya Ahlulbait, tunaoana fahari leo kukabidhi mlango huu kwa watu wa Balad na kwa watumishi wa malalo ya Sab’u Dujail kama zawadi kutoka kwa Abulfadhil Abbasi (a.s) na kwa jina la uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya na watumishi wake, tumeagizwa na kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi tuzitumikie Ataba tukufu daima, Atabatu Abbasiyya tukufu itumie uwezo wake wote katika kusaidia Ataba na malalo mbalimbali”.

Akaongeza kusema kua: “Ilikua siku chungu sana ilipo shambuliwa malalo hii tukufu tena katika mlango wa Hamdi, ambao ni kituo cha waumini na mashukio ya malaika, lakini hili ni jibu kwa kila anaye jaribu kushambulia malalo zetu tukufu, mlango huu umetengenezwa katika kiwanda cha Saqaa, cha kutengeneza madirisha na milango ya malalo tukufu, tumeutengeneza na kuufikisha hapa leo katika malalo ya Sab’u Dujail, tukiwa na salam za Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria pamoja na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, na kamati kuu ya uongzi, pamoja na viongozi wote na watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kutoka katika mji wa shahada na kujitolea mji mtukufu wa Karbala, tunamuomba Mwenyezi Mungu atukubalie hiki kidogo tulicho fanya, tunawashukuru sana watumishi wa malalo ya Sayyid Muhammad (a.s), waliotupa nafasi hii tukufu ya kumtumikia Sayyid Muhammad kwa kutengeneza mlango huu kupitia jina la Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Baada ya hapo wanyama wakachinjwa na kupigwa swalawatu nyingi kutoka kwa wahudhuriaji huku wakinawirisha macho yao kwa kuangalia mlango mpya ulio letwa.

Msafara huo uliongozana na mafundi kutoka katika (kiwanda cha Atabatu Abbasiyya tukufu cha kutengeneza madirisha na milango ya malalo na mazaru tukufu) katika Atabatu Abbasiyya wakiongozwa na Muhandisi Ali Salum, mmoja wa wasimamizi wa kutengenezwa kwa mlango huu ambaye alishiriki pia kuuweka mahala pake, na kuufanya mlango wa Hamdi urudi katika muonekano bora na wa kupendeza, kazi yote imefanywa na wairaq halisi, kuanzia usanifi, utengenezaji na uwekaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: