Atabatu Abbasiyya imemaliza maonyesho ya viwanda vya Iraq na waziri wa viwanda asifia ushiriki wao…

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imemaliza maonyesho ya viwanda vya Iraq ya awamu ya tatu yaliyo pewa jina la (viwanda vya Iraq), yaliyo simamiwa na wizara ya viwanda ya Iraq katika eneo la maonyesho ya kimataifa mjini Bagdad, yaliyo dumu siku tano na kupata ushiriki mkubwa kutoka katika mashirika mbalimbali.

Bendera ya Atabatu Abbasiyya tukufu imepeperushwa na (Shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud, Darul-Kafeel ya uchapishaji na usambazaji, kiwanda cha kutengenezea vifaa vya ujenzi na kiwanda cha kutengeneza kokoto na changarawe) kila tawi limeshiriki kwa kuonyesha bidhaa inazo tengeneza, wameonyesha bidhaa za aina mbalimbali za viwandani na za kilimo.

Ushiriki wao haukua kuonyesha bidhaa peke yake, bali wametumia maonyesho haya kutambulisha mafanikio ya Ataba tukufu katika sekta ya kilimo na viwanda, na maendeleo mbalimbali yaliyo patikana katika sekta tofauti za Ataba, Atabatu Abbasiyya imekua ikitumia fursa hizi kufikisha ujumbe wake mtukufu, na kupaza sauti ya uadilifu na uaminifu wa Abulfadhil Abbasi (a.s), hakika maonyesho haya yalimvutia kila aliyekuja kuyatembelea na walisifu badhaa zilizo kua zikionyeshwa.

Wizara ya viwanda imesema kua maonyesho yalipendeza sana na imetoa wito wa kuendelea kushiriki katika maonyesho yajayo.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imesha shiriki mara nyingi katika maonyesho ya kimataifa ya Bagdad, ambayo ni maonyesho muhimu, pamoja na kushiriki katika maonyesho na makongamano mbalimbali ndani na nje ya Iraq, ambapo hutumia nafasi hizo kuonyesha mafanikio yaliyo patikana katika sekta zake mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: