Baada ya kupata mafanikio Iraq: semina za (Mwenyendo wa haki kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi kitakasifu) sasa zafanyika Landan…

Maoni katika picha
Baada ya kituo cha maarifa ya Qur’an kuifasiri na kuichapisha chini ya maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya kufanya semina za (Mwenendo wa haki kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi kitakasifu) zilizo hudhuriwa na watu mbalimbali nchini Iraq, leo wanafanya semina hizo katika mji kuu wa Uingereza Landan, kupitia tawi la Maahadi ya Qur’an lililopo huko, na kupata washiriki wengi walimu wakike na wakiume miongoni mwa waislamu wanaoishi katika mji huo, watu wenye asili ya mataifa tofauti, wenye asili ya Iraq, Kuwait, Bahrain na Lebanon.

Kwa mujibu wa maelezo ya msimamizi wa semina hiyo Shekh Dhiyaau-Dini Aali Majidi Zubaidi mkuu wa kituo cha maarifa ya Qur’an kuifasiri na kuichapisha amebainisha kua: “Hakika semina hizi ni mwendelezo wa semina zilizo fanywa Iraq na zingine Uingereza, kutokana na kuona kwetu umuhimu wa kubainisha mwenendo huu, kwa kuzingatia kua ndio njia ya uokovu kwa waumini katika zama za fitna, kwani ndio kamba ya Mwenyezi Mungu madhubuti na nuru yake yenye kuongoza ambayo ni Qur’an tukufu na kizazi kitakasifu, simina ilianza kwa mada za utambulisho wa mambo yatakayo someshwa katika semina, pamoja na kugawa kitabu cha (Mwenendo wa haki) ambacho ni moja ya rejea muhimu zinazo tumika katika semina hizi, ili kuwawezesha kupata muongozo katika kuijua haki na kua sawa na taa litakalo waongoza katika njia ya vizito viwili”.

Shekh Zubaidi akaongeza kusema kua: “Tumesha andaa ratiba kamili ya semina hii pamoja na mada zitakazo fundishwa, semina itachukua siku kadhaa, tutafundisha mwenendo wa haki tulio elekezwa na Mtume Mtukufu (s.a.w.w) wa vizito viwili, pamoja na kutoa nafasi ya maswali na majibu, na mwisho wa semina washiriki watapewa jaribio na watapewa vyeti vitakavyo andikwa kiwango alicho pata mtu katika jaribio hilo”.

Dokta Jalalu Feruzi mmoja wa washiriki wa semina hii alisema kua: “Hakika semina hii toka siku za kwanza, ilikua imejaa maarifa mengi na muhimu, tumefaidika sana na tunatarajia irudiwe tena siku zijazo, na mwalimu Zainabu Muhammad akasema kua: “Hakika faida kubwa ya semina hii, inafaa sana kwa mwenye kufanya utafiti wa kutafuta haki kwa kufuata mwenendo wa kitabu na kizazi kitakasifu, na kuweza kubaini imani sahihi na kuifuata, jambo zuri katika semina hii, mambo yote yaliyo fundishwa yako wazi na yanaeleweka, ni muhtasari mzuri uliojaa dalili kutoka katika vitabu maarufu kwa wafuasi wa madhehebu ya Ahlulbait (a.s)”.

Kumbuka kua kituo cha maarifa ya Qur’an kuifasiri na kuichapisha, toka kuanza kwa harakati zake kimejikita katika kubainisha mwenendo wa vizito viwili, kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi kitakasifu, kama vinavyo fafanuliwa na Qur’an, kinatumia uwezo wake wote kwa ajili ya kubainisha swala hilo, wanafanya nadwa, makongamano, mashindano pamoja na kuchapisha vitabu na kufanya semina kama hizi ndani na nje ya Iraq, kupitia Maahadi ya Qur’an tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: