Mwezi tano Jamadal-Ula ilichomoza nuru ya Aqilah bibi Zainabu Kubra (a.s)…

Maoni katika picha
Mwezi tano Jamadal-Ula bibi Fatuma Zaharaa (a.s) alijifungua mtoto mtukufu, mwenye hadhi kubwa katika uislamu kiimani, kiutakasifu na kijihadi bibi Zainabu (a.s), alizaliwa katika nyumba tukufu na mzazi mtakasifu, ambaye ni mbora wa wanawake wa ulimwenguzi bibi Fatuma Zaharaa (a.s), akiwa chini ya usimamizi wa mbora wa viumbe wote Mtume Muhammad (s.a.w.w), na baba yake ni kiongozi wa waumini (a.s), na kaka zake ni Imamu Hassan Al-Mujtaba na Imamu Hussein (a.s), alifumbua macho yake akiwa katika nyumba ambayo kwa ufupi tunaweza kusema kua Jibrilu alikua ndio mtumishi wao kwa amri ya Mwenyezi Mungu.

Alipokelewa na watu wa nyumba ya Mtume (a.s) pamoja na maswahaba wengine kwa bashasha na furaha kubwa, Imamu kiongozi wa waumini akamfanyia kanuni za kisheria, akamuadhinia katika sikio la kulia na kumkimia katika sikio la kushoto.

Hakika sauti ya kwanza kuingia katika sikio lake ilikua ni sauti ya Imamu ya: (Allahu Akbaru, Laailaaha Illa-Llah), maneno haya ni uradi wa mitume, na lulu ya utukufu ulimwenguni.

Maneno hayo yalikita katika moyo wa mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) yakawa kielelezo kikuu cha kuimarisha nafsi yake.

Mtoto wa Mtume (s.a.w.w) akambeba mtoto wake hadi kwa Imamu akamkabidhi, naye Imamu akawa anamgeuza geuza mikononi mwake, bibi Fatuma akamwambia: “Mpe jina mtoto huyu…” Imamu akamjibu kwa adabu na heshima: “Siwezi kumtangulia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w)…” Imamu akampeleka kwa Mtume ili ampe jina, Mtume akasema: “Siwezi kumtangulia Mola wangu mlezi…” Akateremka mjumbe kutoka mbinguni kwa Mtume (s.a.w.w) akamwambia: “Mtoto huyu mwite Zainabu, Hakika Mwenyezi Mungu amemchagulia jina hilo”.

Miongoni mwa sifa zake kubwa ni kuipa nyongo dunia, alijitenga na mapambo ya dunia, akifuata nyayo za baba yake aliye italiki dunia talaka tatu zisizo kua na rejea, pia alimwiga mama yake mbora wa wanawake wa ulimwenguni uwa la Mtume (s.a.w.w), -wanahistoria wameripoti kua- alikua hamiliki katika nyumba yake ispokua mkeka ulio tengenezwa kwa majani ya mtende na ngozi ya mbuzi, na alikua anavaa shuka iliyo tengenezwa na manyoya ya ngamia, na alikua anasaga ngano kwa mikono yake mwenyewe na mengineyo mengi katika dalili za kuipa nyongo dunia.

Hakika bibi Aqilah alipambika na muonekano huo mtukufu wa kujitenga na mapambo yote ya dunia, miongoni mwa zuhudi zake alikua haweki kitu kwa ajili ya kesho, kama ilivyo pokewa na Imamu Zainul-Aabidiin (a.s).

Alikua mtu wa zuhudi na kujitenga na dunia, na hilo lilionekana wazi alipo amua kufuatana na kaka yake Abul-Ahraar (a.s), huku akiwa anafahamu wazi kua atauawa katika ardhi ya Karbala, kutokana na habari alizo simuliwa na baba yake, akaamua kusimama pamoja na ndugu yake kwa ajili ya kuunusuru uislamu na kulinda misingi yake mitukufu, huku akitambua kua kaka yake atauawa na yeye kuchukuliwa mateka na kupata mateso mengi, yote hayo aliyafanya kwa ajili ya kuitumikia dini ya Mwenyezi Mungu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: