Maahadi ya Imamu Hussein (a.s) ya mihadhara ya wanawake yaadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa jemedari wa Karbala bibi Zainabu Kubra (a.s)…

Maoni katika picha
Zainabu kachomoza duniani na ulimwengu umenawirika.

Binti sawa na jua aliye tokana na Fatuma na Haidari.

Kwa jina la Nabii Mukhtari..

Tunahuisha furaha kwa Zaharaa na Karari.. Furaha twaihuisha.

Maahadi ya Imamu Hussein (a.s) chini ya idara ya utoaji wa mihadhara kwa wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu ambayo inatumia haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kama makao makuu yake, haija ishia kwenye kufundisha utoaji wa mihadhara peke yake, bali kuna jambo ambalo limeipa Maahadi umaarufu mkubwa, nalo ni kuadhimisha tarehe za kuzaliwa na kufariki kwa Maimamu wa nyumba ya Mtume (a.s), na kutekeleza kauli ya Imamu Swadiq (a.s) alipo sema: (Huisheni Mambo yetu, Mwenyezi Mungu amrehemu atakaye huisha mambo yetu).

Ilipo fika kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Aqilah bani Hashim bibi Zainabu Kubra (a.s), viongozi wa Maahadi na wanafunzi wao wamefanya hafla ya kuadhimisha tukio hilo tukufu lililo nawirisha ardhi na mbingu kutokana na nuru yake, naye ni mtoto wa Ali na Zahraa na watatu (dada) wa Hassanain (Hassan na Hussein) (a.s) jabali wa subira na uaminifu.

Hafla hii ilipambwa na mambo mbalimbali, kama vile kutoa matamko yanayo sisitiza kupambika na sifa zake, Kaswida pamoja na igizo lililo onyesha kuzaliwa kwa bibi Zainabu (a.s).

Kumbuka kua lengo la kuanzishwa kwa Maahadi hii, ni kuipa nguvu sekta ya tabligh ya wanawake, kutokana na umuhimu wake hasa katika vipindi vya maombolezo, na kutoka katika uwanja mdogo hadi uwanja mpana unao husisha fikra nyingi na matukio mbalimbali na kusaidia kutangaza tukio la Imamu Hussein (a.s) la kudumu kwa njia inayo eleweka zaidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: