Kituo cha uchapishaji cha Alkafeel chafanya matangazo kuhusu miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu…

Tawi la Ataba tukufu katika maonyesho ya kimataifa
Kujitegemea wenyewe ndio sera inayo fatwa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika kutekeleza miradi yake katika sekta mbalimbali, kutokana na kuamini uwezo mkubwa wa kiakili walionao wairaq, wana mifano mingi inayo thibitisha jambo hilo, kituo cha uchapishaji cha Alkafeel chini ya kitengo cha habari na utamaduni hakiko mbali na sera hiyo, toka mwanzo kinafanya kazi kwa lengo la kuhakikisha Atabatu Abbasiyya tukufu inajitosheleza katika sekta ya matangazo, ambayo imeanza kuchukua mwelekeo mpya katika miradi yote ya Atabatu Abbasiyya tukufu na wanatumia njia za kisasa zinazo endana na vifaa vya sekta hiyo.

Mtandao wa Alkafeel uliongea na mkuu wa habari Ustadh Muhammad Aali Taajir kuhusu swala hili naye alikua na haya ya kusema: “Atabatu Abbasiyya tukufu inapata maendeleo katika sekta zake zote, makongamano, nadwa na maonyesho ya kitaifa na kimataifa ni moja ya njia kubwa inayo bainisha na kutangaza mafanikio hayo, kituo cha uchapishaji Alkafeel kimebeba majukumu yote yanayo husiana na matangazo kama vile:

  • - Kusanifu na kuandaa mabambo yanayo endana na mazingira ya kila kongamano au maonyesho, kwa namna ya kuvutia sambamba na hadhi pamoja na utukufu wa eneo husika.
  • - Kusanifu na kuchapisha kadi za mialiko.
  • - Kusanifu na kuandaa zawadi za midani na vyeti vya sampuli na aina tofauti.
  • - Kusanifu na kuandaa majukwaa ya matangazo.
  • - Kuendesha majukwaa ya matangazo ya miradi yote ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kufuata utaratibu maalum.
  • - Kupangilia utendaji katika harakati zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya pamoja na makongamo na maonyesho ya kimataifa na kuweka huduma zote zinazo hitajika.

Akaongeza kusema kua: “Kazi hizi zilikua zinaigharimu Atabatu Abbasiyya pesa nyingi, lakini sasa hivi tunafanya kazi zote tukiwa na watalamu walio bobea na wenye uzowefu mkubwa wa kufanya kazi hizi, jambo linalo pelekea kusifiwa kwa kushain (kupendeza) katika makongamano yote, pamoja na kongamano la kimataifa la kidaktari Alkafeel la kwanza, au maonyesho ya kimataifa ya Bagdad, au maonyesho ya (viwanda vya Iraq), kituo kilikua na picha ya wazi pamoja na nafasi maalum katika shughuli hizi, na kimepeleka ujumbe kua watalamu wa Iraq wanaweza kuingia katika mashindano ya soko, bali tuna uwezo mkubwa zaidi, pia tunaweza kusanifu na kufanya kazi yeyote nje ya Atabatu Abbasiyya tukufu, haya yote yanatokana na baraka za mwenye malalo hii tukufu Abulfadhil Abbasi (a.s), chini ya usimamizi mzuri wa viongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu ambao wanafanya kila wawezale kufanikisha majukumu yao kwa ufanisi mkubwa”.

Mwisho wa maneno yake Ustadh Muhammad Aali Taajir alibainisha kua; kituo hiki kinaweza kukidhi mahitaji katika shughuli zake ndani na nje ya mkoa wa Karbala, unaweza kutembelea ofisi zake zilizopo katika mkoa mtukufu wa Karbala/ mtaa wa Hussein (a.s)/ barabara kuu, au piga moja ya namba za simu zifuatazo: (07602322220/ 07602324000/ 07702666550).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: