Atabatu Abbasiyya tukufu yapata tunzo tano katika kongamano la kielimu la kumi na tisa kuhusu uandishi wa vitabu vya hauza katika mji wa Qum…

Maoni katika picha
Asubuhi ya Alkhamisi ya (7 Jamadal-Ula 1934h) limefungwa kongamano la kielimu la kumi na tisa la waandishi wa hauza, lililofanywa katika mji mtukufu wa Qum na kushiriki Atabatu Abbasiyya na Alawiyya, na makumi ya vituo vya usambazaji na taasisi za dini, elimu na utamaduni zinazo husika na kutoa elimu ya hauza.

Hafla hiyo imehudhuriwa na jopo la wanachuoni pamoja na viongozi wa hauza katika mji wa Qum wakiwemo wageni kutoka katika Ataba tukufu za Iraq, ilishuhudia kupewa zawadi waandishi wa vitabu vilivyo shinda, ambapo Atabatu Abbasiyya tukufu imepata zawadi (tunzo) tano.

Kiongozi wa ugeni wa Atabatu Abbasiyya ulio shiriki katika kongamano hilo, Ustadh Haji Ali Swafaar ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuhusu zawadi (tunzo) hizo kua: “Tulipata mwaliko mtukufu kutoka kwa viongozi wa hauza katika mji wa Qum, wa kuja kushiriki katika kongamano la kumi na tisa la waandishi wa hauza, Atabatu Abbasiyya imeshiriki na kupata tunzo (zawadi) tano ya vitabu vitano, viwili vilipata nafasi ya kwanza na vitatu vikapata nafasi ya pili, pia Ataba tukufu imepewa tunzo ya kua kituo bora cha usambazaji na uhakiki, baada ya wahakiki wake kuchukua sehemu kubwa ya tunzo zilizo tolewa katika kongamano hili”.

Akaongeza kusema kua: “wahakiki na watafiti walikua si wenye kupata nafasi ya kwanza kama sio utukufu wa Mwenyezi Mungu na ulezi mzuri wa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi”.

Akabainisha kua: “Viongozi na wasimamizi wa kongamano hili wameipongeza Atabatu Abbasiyya tukufu, na wameonyesha kuthamini sana mchango waliotoa katika ushiriki wao”.

Mwishoni mwa hafla bendera ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ilikabidhiwa kwa wasimamizi wa kongamano, na kupokelewa na Ayatu-Llah Shekh Jafari Subhani ambaye ndio mkuu wa hauza katika mji mtukufu wa Qum.

Kumbuka kua tunzo (zawadi) tano ilizo pata Atabatu Abbasiyya tukufu, kutoka katika vitabu (1000) vilivyo shindanishwa katika kongamano, kutoka katika taasisi na vituo mbalimbali, ilitokana na vitabu vifuatavyo:

- (Mausua ya Alamah Urdibadi) kilicho andikwa na Shekh Muhammad Ali Urdibadi na kuhakikiwa na mjukuu wake Sayyid Mahdi Shirazi, na kuchapishwa na kituo cha turathi katika maktaba ya Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya, kimepata tunzo kwa kua kitabu bora kilicho hakikiwa.


- (Irabu za Nahju balagha) kilicho andikwa na Ustadh Muhammad Khalil Abbasi Hasanawi, na kuchapishwa na idara ya masomo na usambazaji katika kitengo cha habari na utamaduni, kimepata tunzo ya kua kitabu bora.


- (Muhtasar Maraasimul-Alawiyyah) cha (mhakiki Hilly) na kilihakikiwa na (Ahmadi Ali Majidi Hilly) kikachapishwa na kituo cha turathi za Hilla chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu, kimetata nafasi ya pili.


- (Msahafu mtukufu unao nasibishwa na Ali bun Hilali Al-Bagdadi anaye anajulikana kama Ibun Bawaab) kilicho hakikiwa na Ustadh Ali Swafaar na kuchapishwa na kituo cha upigaji picha wa nakala kale na faharasi chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimepata nafasi ya pili.


- (Muhtasar wa habari mashuhuri kuhusu maimamu kumi na mbili) kilicho hakikiwa na Sayyid Alaa Mussawi na kuchapishwa na kituo cha kuhuisha turathi katika maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimepata nafasi ya pili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: