Kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) chasherehekea ushindi na kuwakumbuka mashahidi wake katika tamasha linalo simamiwa na kikosi cha madaktari wa vitani…

Maoni katika picha
Asubuhi ya leo Juma Mosi (9 Jamadal-Ula 1439h) sawa na (27 Januari 2018m) limefanyika tamasha la kusherehekea ushindi, linalo simamiwa na madaktari wa vitani wa kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) chini ya kauli mbiu isemayo (Ushindi umepatikana kutokana na damu za mashahidi) ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s).

Tamasha limefanyika kumkumbuka Shahidi Muhammad Radhi-Badri Aljuburi, aliyekua mmoja wa watumishi wa kikosi cha madaktari wa vitani, na kupongeza juhudi za madaktari wa kikosi cha Abbasi, tamasha lilifunguliwa kwa Qur’an tukufu, kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukaimbwa wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya, kisha ukafuata ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu uliowasilishwa na katibu mkuu Muhandisi Muhammad Ashiqari, miongoni mwa aliyo sema ni: “Sio siri kwenu yale yaliyosemwa na wataalam kua kutengeneza jeshi lenye nguvu, lazima uwe na watu shujaa waumini wanakesha katika mazingira magumu kwa ajili ya kulinda usalama wa watu wengine, vitu hivyo ni muhimu sana katika uimara wa jeshi, bila shaka uzowefu unaonyesha kua mpiganaji ndiye msingi mkuu wa kuleta ushindi, pamoja na maendeleo makubwa ya kielimu yaliyopo katika ulimwengu wa leo na siraha za kisasa, itakapo kua siraha ya kisasa mkononi mwa shujaa ni tofauti na siraha hiyohiyo inapokua kwa asiyekua shujaa.

Wanajeshi wa Iraq wamepata uzowefu mkubwa katika vita waliyo pigana kwa kushirikiana na Hashdi Sha’abi dhidi ya magaidi wa Daesh, ushujaa na ujasiri wao umeonekana kufuatia ushindi mkubwa walio pata, ambapo pia juhudi za kutibu majeruhi na kulinda roho zao na kupunguza machungu ya wale walio itikia wito wa Marjaa dini mkuu kwa fatwa yake tukufu iliyo linda taifa, imethibiti kwa wote kua uimara wa jeshi sambamba na misaada iliyokua inatolewa na vikundi vya Husseiniyya, ilikua ni sababu kubwa ya kuwapa nguvu wapiganaji wa jeshi la serikali na wale wa kujitolea wa Hashdi Sha’abi, pamoja na uchache wa misaada hiyo lakini iliwapa nguvu zaidi na kuimarisha nafsi zao.

Tumeshuhudia watu wakiwasaidia ndugu zao bega kwa bega katikati ya uwanja wa vita na tumewakuta katika hospitali mbalimbali, walifanya kila aina ya juhudi katika kutekeleza amana na kusaidia majeruhi, madaktari wengi na wauguzi waliuawa kishahidi wakiwa katika kutekeleza majukumu yao matukufu kwa ujasiri na ushujaa mkubwa, wala hatuja sahau namna alivyo pata shahada jemedari mtukufu Muhammad Radhi Aljuburi (Allah amrehem), pongezi kubwa kwenu ndugu zangu hakika hii ni jihadi takatifu kwa ajili ya kulinda taifa na maeneo matukufu, leo hii tunawakumbuka watu waha wema miongoni mwa waumini, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu akubali matendo yao, awarehem mashahidi zetu na awaponye haraka majeruhi zetu, na awape subira ndugu wa mashahidi, hakika yeye ni msikivu na mjibuji”.

Kisha ukafuatia ujumbe wa kamanda wa kikosi cha madaktari ulio wasilishwa na Dokta Usama Abdulhussein, akaelezea historia ya kuanzishwa kwa tawi la madaktari wa kikosi cha wapiganaji cha Abbasi, na nafasi yao katika vita, jinsi walivyo jitolea kwa ujasiri na ushujaa mkubwa ambao haujawahi kuripotiwa katika historia ya madaktari wa vitani, shahidi tunaye mkumbuka leo bwana (Muhammad Raadhi Aljuburi), baada ya hapo ilionyeshwa filamu iliyo elezea kikosi cha madaktari wa vitani na jinsi walivyo tekeleza majukumu yao na huduma walizo pewa majeruhi wakiwa kwenye mahema katikati ya vita, kisha ikaonyeshwa filamu iliyo kusanya matukio muhimu ya jemedari shahidi Muhammad Radha (Allah amrehemu).

Baada ya hapo Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia katibu mkuu wake ikatoa zawadi kwa familia ya shahidi, mwisho wa hafla hiyo ikagawiwa midani na vyeti vya pongezi kwa vikundi na taasisi zilizo kua zikitoa misaada kwa vikosi vya askari.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: