Ujumbe kutoka Ataba mbili tukufu umewasili katika ardhi ya Lebanon na unatoa mialiko kwa watu mashuhuri kuja kushiriki katika kongamano la kimataifa na kitamaduni Rabiu Shahada awamu ya kumi na nne…

Maoni katika picha
Ujumbe kutoka Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya waelekea Lebanon, kutoa mialiko maalumu ya kuhudhuria kongamano la kimataifa na kiutamaduni Rabiu Shahada awamu ya kumi na nne, na kualika wasomi watakao shiriki katika shindano la kiutafiti ambalo hufanywa sambamba na kongamano hilo mwanzoni mwa mwezi wa Shabani.

Katika saa za awali baada ya kuwasili kwa ujumbe huo, umekutana na wasomi wanne maarufu wa kuandika tafiti, miongoni mwa watu hao ni Chif Qadhi Abdulhalim Sharara, kiongozi wa tabligh katika baraza la waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Lebanon, ambaye alionyesha kufurahishwa sana kwa kufikiwa na ujumbe wa watumishi wa Ahlulbait (a.s), na kupewa mwaliko wa kushiriki katika kongamano ambalo kwa zaidi ya miaka kumi linachukuliwa kua ndio mkusanyiko mkubwa wa kitamaduni na kielimu katika ulimwengu wa kiislamu.

Vilevile ujumbe huo ulikutana na msomi mwingine na mtafiti wa kiislamu Shekh Shafiq Jaradi, mkuu wa Maahadi ya Maarifa ya hekima katika masomo ya dini na falsafa nchini Lebanon, amepewa mwaliko wa kushiriki katika shindano la utafiti na ameombwa kuwaalika watafiti wa Maahadi hiyo.

Baada ya hapo ujumbe huo ulikutana na rais wa mahakama za Jaafariyya za Lebanon Mheshimiwa chif-Qadhi Muhammad Kan’an, amealikwa kua mzungumzaji katika kongamano, naye amesifu harakati zinazo fanywa na Ataba tukufu za Karbala katika sekta zote, za kielimu na kitamaduni.

Mtu mwingine walie kutana naye ni Chif-Qadhi Ali Maula ambaye ni mtu maarufu, wakamwalika ashiriki katika shindano la utafiti litakalo fanyika katika kongamano la awamu ya kumi na nne.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: