Ushiriki mkubwa wa semina za Qur’an zinazo fanywa na Maahadi ya Qur’an tukufu tawi la Landan chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu…

Maoni katika picha
Wadau wa elimu na utamaduni wamesifu utendaji wa Maahadi ya Qur’an tukufu tawi la Landan chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, yamesemwa hayo katika hafla ya kufunga semina ya (Mwenendo wa haki ni kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi kitakasifu), ambayo ilikua na washiriki zaidi ya thelathini wakike na wakiume miongoni mwa wadau wa Qur’an tukufu katika nchi ya Uengereza, hafla hiyo ilifanyika katika taasisi ya Ahlulbait (a.s) katika mji mkuu wa Uengereza Landan, na kuhudhuriwa na Mheshimiwa Shekh Rashadi Answari, na mkuu wa chuo cha kimataifa cha elimu za kiislamu Dokta Ibrahim Aati na Sayyid Muhsin Khalkhali pamoja na walimu mbalimbali na watafiti.

Muongozaji wa hafla, Ustadh Muhammad Mudhafar ambae ni mkuu wa Maahadi ya Qur’an tawi la landan, katika maelezo ya awali amebainisha harakati zinazo fanywa na Maahadi Uengereza, kisha hafla ikafunguliwa kwa Qur’an tukufu, iliyo somwa na mmoja wa wanachama wa Maahadi ya Qur’an tawi la Landan (Muhammad Mahdi Mudhwafar) ukafuata ujumbe wa Maahadi ulio wasilishwa na Shekh Dhiyaau-Dini Aali Majidi Zubaidi mkuu wa kituo cha maarifa ya Qur’an kuifasiri na kuichapisha, aliyekua mkufunzi wa semina hiyo, alielezea mafanikio ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kisha ukafuata ujumbe wa Mheshimiwa Shekh Rashadi Answari, ambaye alisifu juhudi za watumishi wa Maahadi, bila kumsahau kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu, Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, na akapongeza mafanikio ya semina hii muhimu, na akasema kua kuna haja kubwa ya semina kama hizi katika nchi za Magharibi, akapongeza sana mafanikio ya Qur’an katika Maahadi.

Hali kadhalika hafla ilipambwa na Kaswida kuhusu mapenzi ya Ahlulbait (a.s) zilizo imbwa na Ustadh Ibrahim Answari, na ujumbe wa washiriki ulio wasilishwa na bi Samira Hassan, ambaye aliishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mafunzo haya na akasifu kitabu cha Mwenendo wa haki, mwisho wa hafla washiriki wa semina wakapewa vyeti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: