Sayyid Swafi: Raia wa Iraq wanaweza kufanya mambo ambayo wengine hawayawezi wana uwezo wa kupambana na mazingira yote, na kwa sasa wako imara…

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmad Swafi, amesisitiza kua wananchi wa Iraq wanaweza kufanya mambo ambayo wengine hawayawezi, na wana uwezo wa kupambana na mazingira ya aina zote, na kwa sasa wako imara zaidi pamoja na hatari zote zinazo wazunguka.

Aliyasema hayo pale alipo kutana na viongozi wa kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) kutoka katika mikoa mbalimbali ya Iraq wakiongozwa na kiongozi mkuu wa kikosi hicho Ustadh Maitham Zaidi.

Sayyid Swafi amezungumza mambo mengi, miongoni mwa hayo ni:

 • 1- Raia wa Iraq wana uwezo wa kufanya mambo ambayo wengine hawayawezi na tuna mifano mingi kuhusu hilo.
 • 2- Matatizo ya Iraq yanatokana na kutokuwepo kwa idara maalum inayo linda na kusimamia rasilimali za nchi tangu kuanzishwa kwa taifa hili mwaka 1920m hadi leo, na hakuna taifa lolote lililo fanya juhudi ya kuisaidia Iraq kiuchumi.
 • 3- Kwa sasa tuna majukumu makubwa zaidi.
 • 4- Raia wa Iraq kwa sasa wanategemea kupata maendeleo.
 • 5- Lazima tuonyesho vipaji na uwezo wa wairaq.
 • 6- Kipindi hiki ni kipindi nyeti (muhimu) sana.
 • 7- Raia wa Iraq wanaweza kupambana na mazingira ya aina zote.
 • 8- Raia wa Iraq kwa sasa wako imara zaidi pamoja na hatari zote zinazo wazunguka.
 • 9- Tumejaribu kutoweka msaada maalum kwa kikosi cha wapiganaji cha Abbasi tofauti na vikosi vingine vya wapiganaji, kwa ajili ya umuhimu wa kuendelea kua kama baba mlezi wa wote, pamoja kua tunafaham tunacho kitoa kwa kikosi cha Abbasi hakitoshi.
 • 10- Kua mwanachama wa kikosi cha wapiganaji cha Abbasi kuna faida, miongoni mwa faida zake ni kua na subira na kutorudi nyuma kuhusu misingi na malengo yetu, pamoja na kuwepo kwa uchaguzi mbalimbali hadi sasa.
 • 11- Subira ni sehemu ya ukamilifu wa mu-umin, Imamu Ali (a.s) alinyang’anywa haki yake kwa mda wa miaka 23, akasubiri na mwisho wa siku alishinda, hali kadhalika maimamu wengine (a.s).
 • 12- Ushindi walio pata kikosi cha wapiganaji cha Abbasi ulikua umepangwa.
 • 13- Pamoja na ushindi wa kikosi cha Abbasi, damu za mashahidi zilizo mwagika vitani bado hazija kauka, na nijukumu la viongozi wa kikosi, ushindi kabla ya shahada ndio lengo letu kuu.
 • 14- Baadhi ya watu walitubana katika maswala ya mishahara ya wapiganaji wa kikosi, hadi leo bado mambo hayajawa mazuri pamoja na kuongea na viongozi na kuahidiwa mambo mazuri, lakini kuna shinikizo kubwa kwao kutoka kwa watu wanaotaka kuondoa uwepo wetu.
 • 15- Watu wema wanakizungumzia kikosi cha Abbasi kwa utukufu na heshima kubwa, kwa sababu kimetoa mchango mkubwa katika kulinda taifa na kipata ushindi mkubwa.
 • 16- Ushindi uliopatikana kwa mikono yenu utaendelea kua sifa nzuri kwenu na kwa vizazi vyenu.
 • 17- Tunaandika mausua (kitabu) kinacho elezea mambo muhimu yote yaliyo tokea vitani na ushindi ulioletwa na watu walio itikia fatwa tukufu, ambacho kitafika juzuu 25, tunahitaji ushirikiano na vikosi vyote vya wapiganaji kwa ajili wa kuthibitisha matukio na habari za kivita, ili kitabu hicho kiwe kielelezo bora kwa vizazi vijavyo, waweze kufahamu namna kungi la kigaidi la Daesh lilivyo shindwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: