Wingu la huzuni ya Fatwimiyya latanda katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)…

Maoni katika picha
Mbingu zimejaa mawingu ya huzuni ya Fatwimiyya.. nyoyo zinahuzunika, korido pamoja na kuta za haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s)..

Huzuni imetanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na imepambwa kwa rangi nyeusi kufuatia kumbukumbu ya kufariki kwa mtoto wa Mtume mtukufu bibi Zaharaa (a.s) kwa mujibu wa riwaya inayo sema alifariki baada ya siku (75) za kufariki kwa Mtume (s.a.w.w).

Zimepandishwa bendera nyeusi na vitambaa vinavyo ashiria maombolezo ndani na nje ya ukumbi wa haram tukufu, na taa nyekundu zimewashwa kwa ajili ya kuadhimisha tukio hili chungu na kutoa pole kwa Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s).

Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalum ya maombolezo inayo husisha mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na utoaji wa mihadhara ya kidini, na kufanya majaalis (vikao) vya maombolezo vinavyo elezea utukufu wa bibi huyu na mitihani aliyo kutana nayo baada ya kufariki kwa baba yake Mtume mtukufu (s.a.w.w), pia Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kua imejiandaa kupokea Mawakibu (vikundi) vya maombolezo kutoka ndani na nje ya mkoa mtukufu wa Karbala.

Tunapenda kufahamisha kua; hakuna tarehe maalum ya kufariki kwake (a.s), kuna riwaya tatu kuhusu kufariki kwake baada ya Mtume (s.a.w.w), kwa hiyo kila mwaka waumini hufanya maombolezo ya kufariki kwake kwa mujibu wa riwaya tofauti, kipindi cha kumbukumbu ya kufariki kwake huitwa (Msimu wa huzuni za Fatwimiyya).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: